Uchaguzi 2020 Mtangaza nia Bara anapata wapi mamlaka kuwaonya watangaza nia Zanzibar?

Kwa majibu mepesi utaambiwa anayo mamlaka kwa sababu yeye ndie mwenyekiti wa ccm taifa, na hapo ametumia mamlaka ya uenyekiti. Lakini kwa maoni yangu naona suala la zanzibar kwa ujumla bado ni nyeti mno.

Kama znz ni nchi je rais wa znz akivuka maji anakuwa na cheo gani?
Kama znz ni nchi je imeungana na nchi gani ili iwe sehemu ya jamuhuri ya muungano?
Kama znz si nchi je kwa nini iwe na rais?
Kama znz si nchi je kwa nini iwe na serikali?

Yaani kuna mambo mengi sana yakufikirisha kuhusu zanzibar.
 
Uwage unaficha upumbavu wako
Huyo ni mwenyekiti wa ccm Taifa nzima
Ulitegemea nini
Hivi kuwa Kibendera ndio mnakosa hata nusu ya Akili kufikiria
Wewe Kwako sifa tu humu JF
Huna lolote
 
Mtu anaingilia mambo ya nchi nyingine si mnaona udikteta huo mnaambiwa kila siku? Zanzibar wana ustaarabu wao na uhuru wao hivyo wasiingiliwe na waachwe wafanye demokrasia. Bara demokrasia imepokwa na mtu mmoja na kuna mazuzu yanashangilia.
Duh.. Ona haka nako
 
Unaongea kihisia na si kwa mujibu wa katiba
 
Kujimwambafy tu,hana lingine kwa sababu anafahamu kuwa ataenda na Nina alipendalo yeye Chimwaga.Na hawatomfanya lolote na hakuna wa kusema hapana.CCM wana halo mbaya kulikoni mnavyoaminishwa.
 
Hata kama kafanya alivyoweza kufanya kuhakikisha fomu za JMT inatolewa fomu moja tuu, jee mamlaka ya kuwa msemaji wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar hadi kutoa maonyo kayatoa wapi?
Zanzibar ni koloni la Tanganyika!
 
Sio kuwapiga mkwara,,ametumia cheo cha mwenyekiti wa chama
Kwanini jukumu hilo asimwachie Mangula maana na yeye ni mgombea kwa sasa?
Au kila kitu lazima aseme yeye?
 
Unaongea kihisia na si kwa mujibu wa katiba
Kwani kiongozi katiba inasemaje?

Ninavyoamini mimi katiba inatambua serikali ya mapinduzi ya zanzibar na serikali ya jamuhuri ya muungano.
Sasa kama znz ni nchi, je imeungana na nchi gani kutengeneza hiyo serikali ya muungano na kwa nini rais wa znz anapovuka bahari na kukanyaga ardhi ya upande mwingine anakuwa waziri asiye na wizara maalum? Na kama znz si nchi, je ni sawa kikatiba kuwepo rais na serikali ya mapinduzi ya znz ndani ya serikali ya jamuhuri ya muungano?

Ebu lete vipengele vya katiba nahitaji na mimi kujifunza, maana naona suala la znz kwa ujumla bado kuna sintofahamu nyingi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…