GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Akizungumza kwa ' huruma ' kabisa huku akikaribia ' kulia ' Mtangazaji ' maarufu ' wa Clouds fm Adam Mchomvu wakati akitoa salamu zake za mwaka wa kuzaliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema kuwa kiukweli mwaka jana hakuwa mmoja wa Watu waliompigia Kura ya Urais na kwamba Kura yake alimpa aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Ngoyai Lowassa.
Mtangazaji huyo hakuishia tu hapo akaenda mbele na kusema kuwa ' anajuta ' ni kwanini hakumpigia Kura Rais Magufuli na kwamba anahisi pengine ' alirogwa ' na nguvu ya safari ya matumaini ambayo kimsingi imeshia tu katika ' kugoma ' na ' kuandamana '.
Mwisho kabisa Mtangazaji Adam Mchomvu akasema kuwa kwa Kipindi hiki tu cha mwaka mmoja ameona mambo makubwa ambayo ana uhakika kabisa kuwa aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa asingethubutu na hata kuweza kufanya hasa kutokana rekodi yake ya ' wasiwasi ' dhidi ya rasilimali za nchi alizonazo.
Kama kawaida yake Mtangazaji Adam Mchomvu huwa hana ' Unafiki ' na akamalizia tu kwa kuwataka Watanzania wote wamuunge mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani alichokifanya tu kwa mwaka huu mmoja ni kikubwa na kwamba miaka minne ijayo Magufuli ataifikisha Tanzania kule inakotakiwa kufika hasa Kimaendeleo.
Binafsi kama GENTAMYCINE nichukuwe fursa hii kumpongeza kabisa Mtangazaji Adam Mchomvu kwanza kwa kuwa ' muwazi ' na ' mkweli ' na pia kuweza kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa Uongozi wake lakini na Watu wengine hasa wale Wana UKAWA hasa CHADEMA nanyi pia igeni hii busara na hekima aliyoionyesha mwenzenu mwana CHADEMA ' kindakindaki ' Adam Mchomvu na nyie mkubali ' Kazi ' za Rais wetu na ikiwezekana si vibaya hata mkizichana chana tu hizo Kadi zenu za CHADEMA na mrejee rasmi CCM kwani CCM ya sasa chini ya Rais Dkt. Magufuli ' imetakata ' na ' mwendo mdundo '.
Happy Birthday Rais wangu Mpendwa na Mkombozi wa Watanzania ' wanyonge ' na ' fimbo ' ya ' mafisadi ' na ' wavivu ' Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, akulinde, akubariki na akupe afya njema.
Akhsante Adam Mchomvu kwa ' kuthubutu '.