Mtangazaji Adam Mchomvu amwomba radhi JPM kwa kutompigia Kura mwaka jana

Mtangazaji Adam Mchomvu amwomba radhi JPM kwa kutompigia Kura mwaka jana

Kwahiyo kampeni ndo zinaanza tena au? Kwani angempongeza tu bila hayo mengine Ujumbe usinge fika? Yeye nani kwani
 
Akizungumza kwa ' huruma ' kabisa huku akikaribia ' kulia ' Mtangazaji ' maarufu ' wa Clouds fm Adam Mchomvu wakati akitoa salamu zake za mwaka wa kuzaliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema kuwa kiukweli mwaka jana hakuwa mmoja wa Watu waliompigia Kura ya Urais na kwamba Kura yake alimpa aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Ngoyai Lowassa.

Mtangazaji huyo hakuishia tu hapo akaenda mbele na kusema kuwa ' anajuta ' ni kwanini hakumpigia Kura Rais Magufuli na kwamba anahisi pengine ' alirogwa ' na nguvu ya safari ya matumaini ambayo kimsingi imeshia tu katika ' kugoma ' na ' kuandamana '.

Mwisho kabisa Mtangazaji Adam Mchomvu akasema kuwa kwa Kipindi hiki tu cha mwaka mmoja ameona mambo makubwa ambayo ana uhakika kabisa kuwa aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa asingethubutu na hata kuweza kufanya hasa kutokana rekodi yake ya ' wasiwasi ' dhidi ya rasilimali za nchi alizonazo.

Kama kawaida yake Mtangazaji Adam Mchomvu huwa hana ' Unafiki ' na akamalizia tu kwa kuwataka Watanzania wote wamuunge mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani alichokifanya tu kwa mwaka huu mmoja ni kikubwa na kwamba miaka minne ijayo Magufuli ataifikisha Tanzania kule inakotakiwa kufika hasa Kimaendeleo.

Binafsi kama GENTAMYCINE nichukuwe fursa hii kumpongeza kabisa Mtangazaji Adam Mchomvu kwanza kwa kuwa ' muwazi ' na ' mkweli ' na pia kuweza kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa Uongozi wake lakini na Watu wengine hasa wale Wana UKAWA hasa CHADEMA nanyi pia igeni hii busara na hekima aliyoionyesha mwenzenu mwana CHADEMA ' kindakindaki ' Adam Mchomvu na nyie mkubali ' Kazi ' za Rais wetu na ikiwezekana si vibaya hata mkizichana chana tu hizo Kadi zenu za CHADEMA na mrejee rasmi CCM kwani CCM ya sasa chini ya Rais Dkt. Magufuli ' imetakata ' na ' mwendo mdundo '.

Happy Birthday Rais wangu Mpendwa na Mkombozi wa Watanzania ' wanyonge ' na ' fimbo ' ya ' mafisadi ' na ' wavivu ' Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, akulinde, akubariki na akupe afya njema.

Akhsante Adam Mchomvu kwa ' kuthubutu '.
Mmh ameomba lini huo msamaha? Mi mdau wa xxl sana tu cjawah isikia hii au hakusema redion?
 
Hapo ashukur kuwa clouds fm vinginevyo asingefahamika man Hanaga hoja za msing au za mashiko, kama hakumpigia ni sir yake yanin kufichuwa, huo ndio umbeya na unafiki, jaman huku kujipendekeza tutapata watu wasio tufaa
 
Kwahiyo kampeni ndo zinaanza tena au? Kwani angempongeza tu bila hayo mengine Ujumbe usinge fika? Yeye nani kwani

Yeya ni Mtangazi mahiri, machachari, mbunifu, mchapa kazi, mwerevu sana, mwenye mvuto na aliyeweza kukusanya kijiji cha Wasikilizaji wengi wa Redio hasa Vijana wanaochangia 65% ya Population ya nchi hii na anakubalika kunakotukuka si tu Tanzania bali hadi huko ' duniani '. Labda na Wewe pia unayehoji kuwa huyu Adam Mchomvu ni nani utuambie kuwa hivi na Wewe ni nani pia?
 
Mmh ameomba lini huo msamaha? Mi mdau wa xxl sana tu cjawah isikia hii au hakusema redion?

Yawezekana aliposema hivyo labda ulikuwa umeenda mara moja kukata ' bogi ' chooni hivyo hukuweza kumsikia. Siku nyingine ukiwa unajua unasikiliza XXL na unaelekea kukata ' bogi ' chooni beba kabisa na redio yako ili uwe unamsikiliza Adam Mchomvu na XXL huko huko.
 
Ndo tujiulize hao waliompigia kura wako wapi?

Hao waliompigia kura ni sisi tusio na vyama ambao ni wengi kuliko wenye vyama. Kumbuka kuwa CCM zaidi ya nusu walimpigia yule wa gia za angani kwa hiyo hata rais Magufuli siyo rais wa CCM bali wetu wote na CCM waache unafiki kuwa ni chaguo lao bali Mungu alimchomekea ili kutuepusha na maangamizi ya Taifa letu.
 
huyo dogo nasikia ana 'mdudu' kitambo. Viemeanza kuchanganya ndo mda wake...poleni mabinti mnaokwenda nae stereo....

Wewe umeshapima na kujulikana hujaathirika? au ndiyo unawatahadharisha wenzako baada ya Jamaa pengine ' kukung'ata ' kwa kukuchapa nao? Nijuavyo Watanzania wote ni ' Waathirika ' watarajiwa ila ni muda tu ndiyo tutakaopishana katika ' kudondoka '.
 
Back
Top Bottom