Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
vilaza darasani hukonda zaidi kuliko wenzao vipanga!Mtangazaji ‘ Kipenzi ‘ cha wengi Cloudstv360 Babie Kabae katika hali isiyokuwa ya kawaida leo asubuhi aliweza kutoa ‘ dukuduku ‘ lake moyoni kwa kumshauri Rais JPM ajitahidi awe anatenga muda kidogo wa Kula Bata / Kujiachia ili asiwe mwenye mawazo mengi na aache kila mara kupenda tu kwenda Kupumzika Kijijini Kwake.
Hii imekuja baada ya Mtangazaji huyo pamoja na wenzake wawili Hassan Ngoma na Samuel Sasali walipokuwa wakijadili ‘ Kauli ‘ ya Rais JPM aliposema kuwa anashangaa ni jinsi gani Watangulizi wake Marais Wastaafu Mkapa na Kikwete waliweza Kuiongoza Tanzania bila ya hata Wao Kuchoka na mpaka leo bado wanaonekana wako ‘ fit ‘ huku Yeye ndiyo Kwanza tu akiwa na miaka mitatu Madarakani lakini anaona ‘ Maluweluwe ‘ na Kuchoka kutokana na ‘ changamoto ‘ ambazo anazipata.
“ Kiukweli nipo tayari hata kumuandalia Rais JPM schedule yake ya Christmas pamoja na Mkewe Mama Janet ili waende tu Kupumzika Mbugani au Zanzibar huku wakiwa wamejiachia kabisa na asifanye Kazi yoyote ya Kiserikali ili atulize akili zake kuliko ambavyo hivi sasa pamoja na changamoto zake bado tu anazizidisha tena kwa kwenda Kijijini Chato ambako nako huko tena hupata changamoto zingine hatimaye anajikuta anaona Urais ni kama mzigo Kwake “ alisema Babie Kabae.
Wakati Mtangazaji huyo akiongea hivyo Wenzake akina Hassan Ngoma na Samuel Sasali wao ‘ walichagiza ‘ zaidi katika hali ya ‘ Utani ‘ kama kawaida yao kwa kusema kwamba akina Mkapa na Kikwete hawakuona ‘ Urais ‘ changamoto Kwao kwakuwa Wao muda mwingi walikuwa wakisafiri Ulaya na Marekani ambapo wakirudi Tanzania basi akili zao huwa zimebadilika kidogo kuliko Yeye JPM ambaye kama akisafiri sana basi ni ama Kampala au Kigali ila sana sana Kijijini Kwake huko Chato Mkoani Geita.
Je unadhani Mtangazaji huyu yuko sahihi au hayuko sahihi kiasi gani kwa hii ‘ Kauli ‘ yake dhidi ya Rais JPM?
Nawasilisha.
Hapana si udini ni uwajibikaji, serikali ya awamu ya Pili na nne zote zilikuwa LegelegeNinaona harufu ya udini!