TANZIA Mtangazaji Maarufu wa RTD Abissay Stephen amefariki dunia asubuhi hii

Apumzike salama
 
Pole kwa tasnia ya utangazaji Tanzania. Hawa ndiyo walikuwa watangazaji wa kweli, wenye kuafuata miiko na utaalam, siyo hawa wa sasa wanajiita watangazaji kumbe ni madalali au wakala wa bidhaa/huduma, chawa wa wanasiasa na wachumia tumbo wa kuposha umma kama kina Maulidi Kitenge. BT Pascal Mayalla tunaomba ukipata muda utuwekee list ya watangazaji wa RTD enzi hizo ambao bado wako hai na wanafanya nini. Wengi wametangulia mbele ya haki, mtu unashidwa kujua uhasilia. Kama huyu mimi sikudhani kama bado yuko hai.
 
Abysai binti yake nilisoma nae naona sasa binti pia yupo TBC safi sana mzee, upumzike kwa amani mzee wetu sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi, ulibahatika kuwa na binti mpole na mtulivu sana.
 
Mchaga atakua kajenga kwao zinga la nyumba. Tusubiri tuone makamera msibani
 
Nakumbuka, kama sijakosea, alishawahi kuwa reporter wa RTD Songea..!!
 
Oscar Ulasa nimesikia akitaja jina hili hili

Walikuwa wakijiuliza mchezaji gani wa KMC ametoka mechi kati ya Yanga v KMC

Ulasa akasema 'ahsante sana Abbysai Steven kwa kunisaidia'

Baada ya kumtext mchezaji aliyetoka

Sasa huyo Abbysai Steven ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…