Mtangazaji Masoud Masoud wa TBC

Mtangazaji Masoud Masoud wa TBC

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,721
Wanamwita manju wa muziki. Huyu ni mtangazaji mkongwe na nguli wa maswala ya muziki na wanamziki, kupitia TBC.

Ukimsikiliza Masoud, utaelewa umuhimu wa specialization katika utangazaji, uandaaji vipindi na uandishi habari kwa ujumla.

Masoud anaelewa ni nini anachofanya na kwa muktadha muafaka.

Ukifuatia simulizi zake kimuziki sio tu zina mizania ya kimantiki bali pia zina mtiririko kama movie fulani hivi inayokushawishi kuendelea kuitazama uone mwisho wake.

Hongera Manju,
MASOUD MASOUD !
 
Ama hakika hili ni gulu la habari za mziki na wanamziki.
Anaujua mziki hasa wa enzi zile sio hawa vijana wa kileo na kelele kelele za bangi.
Kutangaza hawajui ujuaji mwingi, matusi na maisha yao yamegubikwa makandokando mengi.
Cc Adam Mchomvu&B12
 
ndo sukari, gani ya zakaria au, ya kimakonde.
 
Yupo vizuri, ila sijui hapendi exposure yeye, kwa maana hata ya kutoka na kutangaza redio ama tv tofauti na aliyopo.

Ila kuna wakati kama nilikuwa namsikia BBC SWAHILI, miaka kidogo imepita, ila ni kwa muda tu nikamsikia tena karudi TBC

Anaijua vema kazi yake. Hongera yake.

Ahsante!
 
Back
Top Bottom