Mtangazaji wa Efm Maulid Kitenge tumekuvumilia vya kutosha na sasa unatuchosha kama siyo kutuboa

Lakini umemsahau pia Oscar Oscar, anapitiliza unazi wake wa Yanga hasa sakata hili la Kagera.

Oscar Oscra ambaye Kitaaluma ni Mwalimu Shule ya Msingi Wilaya ya Kinondoni ( japo nasikia ameshaachana nao ) ni Mwana Simba Sports Club ' mtupu ' Mkuu lakini je kuna siku yoyote umemsikia akifanya biased analysis katika mambo ya Kimpira hasa huu wetu wa Bongo? Efm Simba ni Ibrahim Masoud ' maestro ', Tunu Hassan Shenkome, Oscar Oscar na Panju Panjuani ILA Yanga FC ni Maulid Kitenge, Yusuph Mkule, Sudi Mkumba, Twalib Omar Muwa, Musa Mwakisu na Francis Mhando.

Habari ndiyo hiyo Mkuu.
 
Tumekusikia na tumekuelewa!!

Vipi maoni yako kuhusu kadi tatu za njano na je mustakbali wa point tatu za dezo??
 
Mleta uzi unaugonjwa mmoja tu,ambao ni 'Kuhalalisha hisia zako' na kutaka kuaminisha watu hisia hizo kuwa ni 'ukweli '.
Kwenye utetezi wako umetumia mfano mmoja tu Kuhalalisha hisia zako,huyo Kitenge kaanza kuwahoji wadau lini?,kaanza kuendesha vipindi lini?...huwezi kutumia tukio moja kuja na HITIMISHO kama hilo.Umesema wewe ni mwandishi kitaaluma...nasikitika sana hivi vyuo vinatoa wataalam kama wewe mnaokariri uandishi kuwa ni subjective perception of reality.

Ongeza Mifano mingine ili uetendee haki uzi wako mkuu, nakuheshimu sana.
 
Juzi kati ulikua na Enock na leo Maulid sijui kesho nani
 
Kwani nyie hamna mkanda wa video wa mechi ambayo mchezaji huyo alipewa kadi hizo ?? au mnataka kupiga ramli tu...!!! Kama kuna kielelezo cha mchezo ambacho kinaonyesha mchezaji huyo hakupewa kadi tuleteeni hapa........!!!!!

acheni kulialia semeni kadi tatu za njano zilipatikana lini sio kutaka point za mezani, jana manara katoa povu weee ila hamna kitu cha maana alichoongea!
 
Kwani nyie hamna mkanda wa video wa mechi ambayo mchezaji huyo alipewa kadi hizo ?? au mnataka kupiga ramli tu...!!! Kama kuna kielelezo cha mchezo ambacho kinaonyesha mchezaji huyo hakupewa kadi tuleteeni hapa...Nyambafu.....!!!!!
hiyo mechi ambayo simba wanalilia kuwa fakhi alipewa kadi ni ile ya african lyon ambayo haikuoneshwa kwenye tv wala kwenye rekodi za refa hakuna kitu kama hicho sasa sijui simba wanatoa wapi nguvu ya kulilia point za mechi waliyofungwa!
 
Huyo Dada ndiyo ' takataka ' kabisa Mkuu. Ndiyo maana kanenepeana hovyo kama ' Faru Fausta '.
Mkuu kwanini unamshambulia yeye binafsi hasa umbo lake, Kwani linahusiana nini na hiyo tabia usiyo ipenda?
 
Sasa nyie mnauhakika gani kama yule mchezaji hakupewa KADI ikiwa hiyo mechi haikuoneshwa wala hakuna report nafikiri wa kulaumiwa ni bodi ya ligi na TFF kwa kutokuwa na video ya mechi hiyo.

hiyo mechi ambayo simba wanalilia kuwa fakhi alipewa kadi ni ile ya african lyon ambayo haikuoneshwa kwenye tv wala kwenye rekodi za refa hakuna kitu kama hicho sasa sijui simba wanatoa wapi nguvu ya kulilia point za mechi waliyofungwa!
 
Sasa nyie mnauhakika gani kama yule mchezaji hakupewa KADI ikiwa hiyo mechi haikuoneshwa wala hakuna report nafikiri wa kulaumiwa ni bodi ya ligi na TFF kwa kutokuwa na video ya mechi hiyo.
mkuu kwenye sheria wanasema yule anayeshutuma ndio anapaswa kuthibitisha, na kwa kesi hii simba ndio mwenye jukumu la kuthibitisha hiyo kadi ilitoka mechi gani na dakika ya ngapi kwa kushindwa kufanya hivyo watakua hawana haki ya kulalama, kuhusu bodi ya ligi na tff hayo ni majipu makubwa na hivi sasa ni siasa za uchaguzi ndio zimetawala!
 
Mimi simba ila na ww mwenzangu umezidi kila siku wewe na watangazaji tuuu khaaa
 
Kelele za nini tena?!

Tuliungana kwa pamoja kumlazimisha Bashite aweke vyeti hadharani sasa tumeungana tena kuwalazimisha Mikia kurudisha point 3 halali za Kagera Sukari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…