Mtani unauona lakini usajili unaofanywa Simba SC?

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Zifuatazo ni silaha zilizotua Msimbazi;

1. Peter Mwalyanzi
Kiungo fundi toka Mbeya City, shughuli yake Kaseke anaifahamu, mana alimsihi sana wasiende timu moja kwa kuwa benchi lingemhusu.

2. Mohamed Fakhi
Beki katili toka JKT Ruvu. Shughuli yake kina Tambwe, Kipre, Msuva, Maguli wanaijua.

3. Samir Nuhu
Alikua beki tegemeo Azam msimu wa 2013/14 na aliondolewa kwa fitina za kina Ongala. Sasa shughuli anaileta Simba SC.

4. Mohamed Abraham
Huyu alikua kipa tegemeo JKU na timu ya taifa ya Zanzibar. Sasa anakuja kuwachalenji makipa bora kabisa nchini Ivo na 'mwanaye' Manyika.

5. Musa Hassan "Magoli" Mgosi
Huyu ni kiboko ya timu za Dar. Maana msimu uliopita alizifunga zote.

6. Mavugo
Huyu ni mshambuliaji hatari sana toka Burundi anachezea Vitalo, muda si mrefu atasaini. Msimu uliopita alifunga goli 29 katka mechi 29. Rekodi hazidanganyi!

Ikumbukwe tumepandsha wachezaji 3 toka Simba B, na usajili bado unaendelea.

Ama kweli "SIMBA HII NI BAB'KUBWA".
 
Good, ila je usajili huu ni kwa mujibu wa matakwa ya kiufundi au uongozi??
 
Good, ila je usajili huu ni kwa mujibu wa matakwa ya kiufundi au uongozi??

Hayo ni mapendekezo ya Benchi la ufundi, ambalo kwa sasa linaongozwa na Suleiman Matola.
 
Hayo ni mapendekezo ya Benchi la ufundi, ambalo kwa sasa linaongozwa na Suleiman Matola.

Kama ni hivyo ni poa. ila Matola ni msaidizi na hatujui hatma ya kocha mpya. Sasa itategemea pia na kocha mkuu atavyokuwa anataka
ila usajili mzuri
 
Hayo ni mapendekezo ya Benchi la ufundi, ambalo kwa sasa linaongozwa na Suleiman Matola.

Hata hao waliochemsha tuliambiwa ni mapendekezo ya kocha
 
Msimu ujao mjikazekaze walau muangukie hata nafasi ya pili
 
Mgosi?

Yale Yale ya kisiga

Mkuu Mgosi yupo vizuri sana kwa sasa, pia hata tabia yake iko poa.. kupitia Mgosi "magoli" kina ajibu, mkude n.k watajifunza mengi sana tofauti na kwa Kisiga aliyekua akiwapotosha.
 
Mgosi kasajili ili kuwamotivate vijana. He quite different from Mania Smoker i.e Kisiga ambaye badala kuwamotivate yeye aliwademotivate

Watu mnasahau mapema sana kwani Mgosi,Kaseja na Kiemba waliondoka vipi Simba,tatizo kubwa la Simba ni uongozi na sio wachezaji
 
Watu mnasahau mapema sana kwani Mgosi,Kaseja na Kiemba waliondoka vipi Simba,tatizo kubwa la Simba ni uongozi na sio wachezaji

Yupi anafaa kuwepo sasa? Make simba inahitaji wachezaji wenye umri mkubwa wa kuwasidia vijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…