Mtanzania achagua kuichezea timu ya taifa ya Marekani

Mtanzania achagua kuichezea timu ya taifa ya Marekani

Mtanzania anaishi vipi kwenye kambi ya wakimbizi huko kigoma? Kambini wanaishi wakimbizi iweje awe m Tz , embu mwache akajitafutie rikizi bongo kwenyewe kumejaa majungu tu.
 
BERNARD KAMUNGO, Mwanasoka ambaye alilelewa kwenye kambi ya Wakimbizi huko Kigoma, Tanzania! Aliyekuwa na uwezo wa kucheza timu ya taifa ya Tanzania, sasa ameitwa rasmi timu ya taifa ya Marekani kuelekea kambi ya Olympic, uwezekano mkubwa kwasasa ni kuwa tayari ataiwakilisha Marekani huku klabu yake ya FC Dallas ikisema ametoka Kambi ya wakimbizi bila kuitaja nchi, another talent imechagua bendera tofauti na Tanzania.

Hii ni aibu kwa shirikisho letu kwa kushindwa kumpatia nafasi mchezaji aliyekuwa tayari kulitumikia taifa letu mara zote alizoitwa timu ya taifa alikuja lakini hakuwahi kupewa nafasi zaidi alihishia bench na jukwaani hatujui nini kilikuwa kinandelea. Mbaya zaidi nafasi anayocheza kuna watu wanaitumikia lakini uwezo wao ni mdogo sana ila hatujui vigezo gani vinavyowapa hyo nafasi.

Ni kipaji kikubwa sana tumekiacha kiondoke kilahisi hivi huku tukiwa na mashindano makubwa mbele yetu. Sitaki kuamini kama mzize,bocco,kibu,samatta wa sasa wanauwezo mkubwa zaidi kuliko BERNARD ? Hapana nadhani kuna kitu hakipo sawa na hili linaweza kuwa tukio sawa la MBAPE NA KAMERUNI japo sina uhakika. Nenda BERNARD kapambanie ndoto zako miyoyoni kwetu utabakia kuwa mzalendo wa kweli ila tuliamua kukupuuza kwa Ubinafsi tu na roho zetu.

View attachment 2776520
Amefanya jambo la heri sana. Nampongeza maana atacheza World Cup ya 2026 hapohapo Marekani
 
Kwa hiyo watanzania siku hizi mnalea wananchi wenu ndani ya Kambi za Wakimbizi?
Halafu kwanini uwalaumu TFF kwenye hilo swala? Kwanini usiwalaumu wanaokataa kutoa dual citizenship?
Ungekuwa wewe ungerudi kuja kuchezea bongo?
Hata Kalimagonga Ongala aliyelelewa na kukulia hapo Sinza alipofikisha umri wa kuchagua uraia alirudi Uingereza kuchukua uraia wa nchi aliyozaliwa.
Halafu analilaumu Shirikisho la soka.
 
Angekua zwazwa kurudi kucheza ndondo wakati kashafika nchi ya maziwa na asali.
 
Naona kwenye thread mleta mada umesema amewahi kuitwa timu ya Taifa na hakupewa nafasi, ni kweli kabisa ilikua hivii??
 
Mwache kijana atafute maisha.

Watz wenyewe wakipata uongoz wanawapa watoto uraia wa Marekani, ije kuwa mrundi wa Kasulu.
Umesema ukweli; watoto wa viongozi karibu wote wa Tanzania sasa ni raia wa Marekani. Kwa nini mkimbizi asiwe raia wa Marekani? Huyu klijana aliitwa timu ya Taifa ya Tanzania ila alikuwa keshaachukua uraia wa Marekani. Kwa vile Tanzania hairuhusu uraia pacha, ikawa ngumu kwake ingawa timu yake huko Texas ilikuwa imeshampongeza.
 
Hivi Marekani hakuna michezo ya draft na mimi nikajaribu bahati yangu? Maana hapa kijijini kwetu nimekosa mpinzani kabisa, hasa baada ya Mzee Mwakifulefule Atufigwege kuchukuliwa na watoto wake kwa ajili ya matibabu huko mjini, nimekosa mpinzani kabisa.
Huku Marekani hiyo michezo ya wachawi Hakuna,badilisha kipaji uniambie nije kukupakia kwenye ndege.
 
Back
Top Bottom