Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
ConstantineJ. Samali Mauki
Utangulizi
Kila mara huwa nawaza, ikiwa serikali itatekeleza sheria zake kuhusu malipo ya kodi za ardhi na majengo kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kupiga mnada viwanja/nyumba ambazo hazazijalipiwa, ni Watanzania wangapi watakosa makazi na kwenda kuishi mitaani? Sipati majibu sahihi, lakini najaribu kukumbuka kile kipindi cha Kodi ya Maendeleo (zamani ikiitwa Kodi ya Kichwa) ambayo ilikuwa ikitozwa na halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya kwa kila mwanaume mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea.
Ikifikia wakati ambapo serikali itatumia nguvu nyingi kama ilivyokuwa kwa kodi ya maendeleo, kukusanya kodi hizi (ardhi na majengo), watu wataacha miji yao na kwenda kuishi mitaani.
Watu waliozaliwa miaka kati ya 1990 na 2005, hawakushuhudia kero za kodi hii ya Maendeleo, maana kipindi hicho, aidha walikuwa ni watoto wadogo au walikuwa bado hawajazaliwa. Ni vizuri vijana hawa kupiga picha ya hali ilivyokuwa huko nyuma, na hali inavyoweza kuwa sasa na baadaye kuhusiana na tozo mbalimbali za moja kwa moja.
Kilelezo Na. 1: Baadhi ya Makazi Nchini Tanzania
Chanzo: Google: Makazi Tanzania
Kodi ya Maendeleo Ilikuwa Kero Kubwa
Kodi ililipwa kwa shida, ingawa kwa ujumla ilionekana kama ya kiwango kidogo ambapo ingeweza kulipwa na kila mhusika. Kipindi cha kukusanya kodi hii, wakuu wa kaya wengi hasa vijijini, walikuwa wanaikimbia miji yao na kwenda kujificha maporini, na hivyo kushindwa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa manufaa ya familia zao na taifa kwa ujumla. Kwa upande wa mijini, baadhi ya watu waliogopa kwenda maeneo ya umma, kama masokoni, na hata mitaani kwa kuhofia kukamatwa na watoza kodi na kulazimishwa kulipa au kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kodi ya Maendeleo Ilifutwa
Kero za utozaji wa Kodi hii ya Maendeleo zilishuhudiwa nchi nzima, jambo ambalo lilizorotesha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla, kwa sababu wananchi wengi (hasa wa vijijini) walitumia muda mwingi kukimbia watoza kodi, badala ya kutulia na kufanya kazi za uzalishaji. Kero hizi ndio zilimfanya Raisi wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa, kufuta rasmi kodi ya Maendeleo, katikati ya mwaka 2000. Kufutwa kwa kodi hii, hakukusababisha athari yoyote katika uendeshaji wa serikali za mitaa nchini, kwa sababu serikali ilikuwa imeshapata vyanzo mbadala vya mapato kwa ajili ya kuziba pengo hilo.
Hayati Mkapa hakukurupuka kuifuta kodi hii, maana, ikumbukwe kodi hii ilikuwepo toka enzi za ukoloni; awamu mbili kabla yake na kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wake; alitambua uwepo wa vyanzo vingine vingi vya mapato, na kuvifanyia kazi, ambapo fedha za kutosha zilipatikana na hivyo kufidia pengo la kodi hii.
Kodi za Ardhi na Majengo ni Hatari kuliko Kodi ya Kichwa!
Wakati wa utozaji wa Kodi ya Kichwa, watu walikimbia miji yao na/au kuwakwepa watozo kodi mitaani na maeneo ya umma, lakini miji yao iliendelea kubaki salama na waliendelea kuimiliki. Watoza Kodi ya Ardhi/Majengo hawatashughulika na watu, bali na viwanja/majengo, ambapo wakifikia hatua ya kuviuza, watu watakosa makazi yao ya kudumu, na kuishi mitaani.
Kwa nini kodi hii ni hatari zaidi? Kwa sababu, katika familia, kuna watoto, wanawake, wazee, walemavu, wagonjwa, na kadhalika. Makundi haya yatakosa Chakula, malazi, na mahitaji mengine ya msingi; hali itakayosababisha njaa, magonjwa (ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza), kuathirika kisaikolojia, na kadhalika. Mbali na familia nyingi kuathirika moja kwa moja, vijiji na mitaa nayo itaathirika kwa kiasi kikubwa: kutakuwa na uchafuzi wa mazingira, magonjwa ya mlipuko, nk. Kwa upande mwingine, serikali itaanza kuhangaika na swala la watu wasiokuwa na makazi kwa kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili hiyo.
Kodi za Ardhi na Majengo Zinaweza Kufutwa Bila Kuleta Athari za Mapato Kwa Serikali
Pamoja na uwepo wa kodi hizi; kodi za Majengo (“Property Tax”) na Ardhi (“Land Rent”), toka enzi za ukoloni, bado zinalipwa kwa kiasi kidogo, kwani wamiliki wengi wa ardhi/nyumba wana vipato vya chini, na hawajui umuhimu wake. Ukweli huu unathibitishwa na chapisho la Merima Ali, na wenzake (2018), kufuatia utafiti uliofanyika Jijini Dar-es-Salaam na Manispaa ya Mtwara Oktoba, 2017. Kwa muktadha huu, kufutwa kwa kodi hizi hakutaathiri uendeshaji wa shughuli za serikali, maana kuna vyanzo vingi ambavyo vinaweza kuleta mapato makubwa zaidi kuliko yale yanayopatikana kupitia kodi hizi.
Tuwe na Mtizamo wa Hali ya Kizazi Kijacho Kwa Miaka Mingi Ijayo
Ingawa watu wengi hawalipi kodi hizi, (achilia mbali kodi ya majengo ambayo kwa sasa inalipwa kila mwezi kupitia bili ya umeme wa “Tanesco” – kwa viwanja/nyumba zinazopata huduma hii) kwa sasa bado zinaonekana za kawaida; lakini ni muhimu kupiga picha ya miaka ya mbele (miaka 100 na kuendeleza). Kwani, kwa mujibu wa chapisho la “EH Encyclopedia” nchini Marekani, pamoja na kodi nyingine, kodi za ardhi/majengo zilianzishwa mwaka 1796 (mpaka leo Julai, mwaka 2023, ni jumla ya miaka 227 imepita), ambazo ziliendelea kufanyiwa maboresho kulingana na wakati na ukuaji wa uchumi. Kwa mujibu wa chapisho hili, mwanzoni mwa miaka ya 1900, wananchi wengi nchini Marekani walipinga vikali tozo hizi; serikali ilendelea kuzifanyia marekebisho, lakini mpaka leo watu wengi hususani wale wa kipato cha chini wanaendelea kuzipinga.
Kielelezo Na. 2: Wamarekani Wasio na Makazi ya Kudumu Nchini Marekani
Chanzo: Google: “Homeless in USA”
Wakati kodi hizi zinaanzishwa zilikuwa za viwango vya chini, na hivyo hazikuwafanya watu kuacha nyumba zao na kwenda kuishi mitaani; lakini kadri miaka ilivyopita, viwango vilipanda; na sasa kila mwaka kuna watu wanaacha nyumba zao na kwenda kuishi na kuteseka mitaani kutokana na kushindwa kulipa kodi hizi.
Mapendekezo
Serikali ifute kodi za ardhi na majengo; ibaini maeneo mapya na ya kimkakati ya kutoza kodi, ikiwa ni pamoja na kuwezesha uwekezaji wa miradi mikubwa ya utalii, madini, gesi asilia, kilimo, nk.
Serikali iunde timu ya wataalamu wabobezi katika sekta mbalimbali kubaini kodi zilizo kero kwa wananchi, na kubuni vyanzo vipya endelevu vya mapato.
Hitimisho
Serikali iwezeshe watu wake kutumia rasilimali nyingi zilizopo nchini kuzalisha bidhaa na huduma mbalimbali, na kuuza nje na ndani ya nchi, ili pamoja na maendeleo yao, iongeze mapato ya nchi.
Marejeo
CUP London (1969), “Tanganyika under German Rule 1905-1912”
“eh.net/encyclopedia, History of Property Taxes in the United States”
Merima Ali, Odd-Helge Fjeldstad na Lucas Katera (2018), “Property Owners’ Knowledge and Attitudes Towards Property Taxation in Tanzania”

Upvote
7