Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Abiria mmoja Mtanzania amekamatwa juzi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi nchini India, baada ya kukutwa akiwa amebeba dawa za kulevya aina ya cocaine.
Msafiri huyo aliwasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia na dawa hizo zilikuwa zimewekwa kwenye chupa tatu za pombe kali aina ya Whiskey.
Maafisa wa Forodha wa India wamesema kuwa hii imekuwa njia mpya inayotumika sana kusafirisha dawa za kulevya, kwani pombe wanayoitumia (liquor)huyeyuka kwenye uwazi hivyo dawa hizo hutolewa kwa urahisi.
Chanzo: Kitenge Updates