Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya India

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259

Abiria mmoja Mtanzania amekamatwa juzi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi nchini India, baada ya kukutwa akiwa amebeba dawa za kulevya aina ya cocaine.

Msafiri huyo aliwasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia na dawa hizo zilikuwa zimewekwa kwenye chupa tatu za pombe kali aina ya Whiskey.

Maafisa wa Forodha wa India wamesema kuwa hii imekuwa njia mpya inayotumika sana kusafirisha dawa za kulevya, kwani pombe wanayoitumia (liquor)huyeyuka kwenye uwazi hivyo dawa hizo hutolewa kwa urahisi.

Chanzo: Kitenge Updates
 
Bahat mbaya tu mwana atatoka .Ajira hamna raia wanajiongeza
 
Kwenye pesa akili inafanya kazi to maximum..hizo mbinu ni balaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…