Mtanzania akutwa amekufa ndani ya nyumba yake huko Minnesota.

Mtanzania akutwa amekufa ndani ya nyumba yake huko Minnesota.

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2007
Posts
1,439
Reaction score
55
Kuna habari ambazo bado ninazifuatilia kuwa kuna mtanzania amekutwa amekufa ndani ya nyumba yake baada ya Polisi kuvunja mlango. Ninajaribu kufuatilia kupata habari kamili.
 
Kuna habari ambazo bado ninazifuatilia kuwa kuna mtanzania amekutwa amekufa ndani ya nyumba yake baada ya Polisi kuvunja mlango. Ninajaribu kufuatilia kupata habari kamili.
Nitajie jina la huyo mtu nifuatilie hii habari.
 
Mkuu si ungetoa maelezo kidogo juu wasifu wake ili kidogo iwe rahisi hata kufuatilia.
 
Nasikia anaitwa swalehe Msuya lakini sina details zozote kwa hiyo sitaki maswali!
 
Nasikia anaitwa swalehe Msuya lakini sina details zozote kwa hiyo sitaki maswali!

Mkuu Minnesota ni jimbo so ungejaribu kuwa specific na sehemu kama ni Minneapolis or another city...etc
Hata kama hautaki ku-ulizwa!
 
halafu na ninyi ''wazee wa majuu''!.....jaribuni kuzitofautisha posts za siasa na hizi nyingine za kawaida.mnatupa stresses bure tu,EBO!

damn it!
 
Kuna habari ambazo bado ninazifuatilia kuwa kuna mtanzania amekutwa amekufa ndani ya nyumba yake baada ya Polisi kuvunja mlango. Ninajaribu kufuatilia kupata habari kamili.

Mods, pelekeni hii habari kunakohusika, nadhani hapa si mahali pake!
 
Nasikia anaitwa swalehe Msuya lakini sina details zozote kwa hiyo sitaki maswali!

Swalehe Msuya?

Alikuwa mwandishi wa habari "Daily News," Dar es Salaam, na akina Godfrey Mwakikagile, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mhango, Abdallah Ngororo, Charles Kizigha, Kassim Mpenda, Juma Penza, Philip Ochieng', Joseph Mapunda, Costa Kumalija na wengineo in the early seventies.

Alihamia lini USA?

Ikiwa habari hizo ni kweli, poleni sana ndugu zake na rafiki zake.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
 
Last edited:
nashindwa kutoa pole kwani habari zenyewe bado hawajathibitisha bwana

ila poleni ndugu wafiwa kama habari ni ya ukweli mola aiweke roho ya marehemu pema peponi

Amen

Now you're talking! Poleni wafiliwa wote....Mungu amlaze Mtanzania mwenzetu mahali pema peponi.
 
Swalehe Msuya?

Alikuwa mwandishi wa habari "Daily News," Dar es Salaam, na akina Godfrey Mwakikagile, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mhango, Abdallah Ngororo, Charles Kizigha, Kassim Mpenda, Juma Penza, Philip Ochieng', Joseph Mapunda, Costa Kumalija na wengineo in the early seventies.

Alihamia lini USA?

Ikiwa habari hizo ni kweli, poleni sana ndugu zake na rafiki zake.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Swalehe Msuya ninayemfahamu mimi ni accountant, na alikwenda huko US kusoma MBA kama 5 or more years ago, na ninavyojua anaishi huko. Kama habari haitoshi usiweke hapo majina unatuchanganya bure wengine.
 
In any case kama kuna Mtanzania amefariki huko pole kwa wafiwa!
 
ila nasisitiza mlio huko jamani leteni full report huyu ni ndugu yetu na sisi ni wamoja
 
jamani hii post mbona kama imeingilia mlango wa kikeni?
kama hiyo ni sawa basi jana kuna mtanzania mwingine amefia malawi sehemu za chinteche.hapo je? Mwaonaje.........
 
jana kuna mtanzania mwingine amefia malawi sehemu za chinteche.hapo je? Mwaonaje.........

Huyo naye kiherehere sasa shinteshe amefuata nini?halafu ukifia Afrika sio habari bora angefia mineapolisi merekani ndio dili.
 
Swalehe Msuya ninayemfahamu mimi ni accountant, na alikwenda huko US kusoma MBA kama 5 or more years ago, na ninavyojua anaishi huko. Kama habari haitoshi usiweke hapo majina unatuchanganya bure wengine.

Kuna wakati Professor Joseph Mbele aliandika machache mtandaoni kuhusu Swalehe Msuya na alimwita "Mzee Msuya." Sijui huyo Swalehe Msuya unayesema alikwenda shuleni Merikani miaka mitano iliyopita ana umri gani.

Professor Mbele, kutokana na alivyoandika, ni wazi kwamba alimfahamu sana Swalehe Msuya kule Minnesota. Professor Mbele mwenyewe anafundisha Minnesota. Na Swalehe Msuya huyo alihusika na gazeti la "Mshale" linalochapishwa Minnesota. Na bila shaka ni yule aliyekuwa mwandishi wa habari,"Daily News," Dar, miaka ya 1970s.

Ndiyo Swalehe Msuya huyo ninayemzungumzia. Hata mimi niliwahi kuonana naye Dar es Salaam miaka ile ingawa sikuwa mwandishi wa habari pale gazetini.
 
Nimejulishwa ni yule Swalehe Msuya aliyekuwa gazetini, "Daily News," na pia kwamba Professor Mbele ndiyo huyo aliyemzungumzia na walifahamiana sana.

Alikuwa na umri wa zaidi (kidogo) ya miaka sitini. Namkumbuka miaka ile alipokuwa "Daily News."

Mtapewa taarifa zaidi.
 
Back
Top Bottom