Swalehe Msuya amefariki. That can be confirmed. Lakini I don't know who it is exactly. Nafahamu alikuwepo Swalehe Msuya mmoja ambaye alikuwa anasoma Tambaza Sekondari.alikuwa prefect.
Swalehe Msuya uliyemtaja alikuwa lini Tambaza?
Nilikuwa Tambaza High School, Form V - Form VI, 1969 - 1970, lakini sikumbuki kulikuwa na prefect mwenye jina hilo.
Imethibitishwa kwamba Swalehe Msuya aliyefariki kule Minniesota, USA, ni yule aliyekuwa mwandishi wa habari, "Daily News." Waandishi wenzake walio hai wanamkumbuka. Na nimesikia kwamba mdogo wake labda atakwenda Minnesota kuleta maiti ya marehemu Tanzania.
Nilipomwona kwa mara ya kwanza alipokuwa mwandishi pale gazetini, ilikuwa hiyo ndiyo ya mara kwanza nilipoiona sura yake. Angekuwa shuleni na sisi Tambaza, 1969 - 1970, hasa kama prefect, ningemkumbuka. Na kama alisoma Tambaza, ilikuwa kabla ya miaka hiyo.
Haiwezekani marehemu huyo alikuwa Tambaza baada ya 1969 au 1970. Umri wake haulingani na wanafunzi waliokuwa Tambaza baada ya 1969 au 1970. Pia marehemu alikwenda chuoni, Mlimani, kabla ya mimi kwenda kusoma pale, ambako sijui alisomea nini ingawa alimaliza masomo yake na kupata shahada yake - pia sijui mwaka gani.
Umri wa marehemu ni zaidi ya miaka sitini, ingawa sidhani ni zaidi ya miaka sitini na tano.
Bado naikumbuka sura yake, na nilipomwona Dar, nilijua alinizidi umri.