Mtanzania, Alphonce Simbu ashika nafasi ya tatu Marathon IAAF LONDON

Kukaa jukwaa moja na Kenya,Ethiopia kwenye riadha si jambo rahisi. Hongera zako Alphonce Simbu. World Championship Bronze Medallist!
Ila yule mkenya hatari....anapumzi za ajabu.....yaani amemaliza kama ndio anaanza....Yule Muethiopia ameponea chupu chupu kupitwa na Simbu....Zingeongezeka Kilomita kadhaa pale alikuwa chali maana alishaanza mawenge.
 
Mtanzania Joseph Simbu ashika nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya raidha (IAAF) huko jijini London.

Simbu amepambana sana sana na kukaribia kushika nafasi ya pili
Nilikuwa naangalia hapa ila daah wakenya wanakimbia bwana .

Lakini hongera sana mtanzania kwa kuja na medari angalau....
 
hongera zake kwa kupeperusha vyema bendera.
 
Huyu kijana tumuombee siku moja afute ile kauli ya Mzee Mwinyi
 
Ila yule mkenya hata....anapumzi za ajabu.....yaani amemaliza kama ndio anaanza....Yule Muethiopia ameponea chupu chupu kupitwa na Simbu....Zingeongezeka Kilomita kadhaa pale alikuwa chali maana alishaanza mawenge.
Huyo Kirui balaa. MuEthiopia alishatepeta, kungekuwa na extra 5M tu angepitwa na Simbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…