Mtanzania, Alphonce Simbu ashinda Medali ya Dhahabu Mumbai, India

Ndugu taarifa yako haijakamilika.., ameshinda mashindano gani, yameandaliwa na nan, washiriki walikua wangapi etc.. uje utueleze vzr
Alphonce Felix Simbu kawa mshindi wa kwanza na Magdalena Crispin naye ni Mtanzania kawa mshindi wa nne katika mashindano ya STANDARD CHARTERED MUMBAI MARATHON kapata kitita cha $67 elfu .

Alidhaminiwa na DSTV MULTCHOICE TANZANIA.Nafikiri huyu ndio alishika nafasi ya nne kwenye Olympic Marathon mwaka jana
 
Hapo sasa wizara na viongozi wa michezo wa bongo ndipo utapowataka. Ataandaliwa kila namna ya tamasha, tulime kisha tuvune, tusisubiri kuvuna bila kupanda
 
Hengera kwake, tuanze taratibu kurudi kwenye nuru yetu ya miaka ya 70
 
Mbona Nape huyo hatukumuona kumpa Bendera ya Taifa?Utashangaa akirudi wanamuandalia Tafrija,lakini kwenye maandalizi waliingia mitini,
Nape,Nape Napeeee!!
 
Hongera sana kwake, huyu jamaa ninaamini atavunja rekodi zote za wanariadha waliotanguliwa, anabidii sana na mazoezi na anaipenda riadha. Hongera sana Simbu, mkeo na mwanao wanakusubiri kwa hamu sana ile furaha waliyokuwa nayo pindi uliposhinda nafasi ya nne kwe marathoni ile iliyopita now wamefrahi zaidi.. Tusubiri kina Bayi waje na siasa zao tena.
 
Hongera kwa dstv...waliomzamini...akaweza kufanya mazoezi..well done
 
Mwanzo mzuri, roma haukujengwa kwa siku moja, Olympic ijayo utafanya mambo makubwa sana.

Hongera sana kwa kupeperusha bendera ya Taifa, though najua kwa kutokuona umuhimu hakukupatia kwa mbwembwe kama wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…