benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Msichana wa Kitanzania, Zamana kutoka kijiji cha Irente Juu, Kata ya Magamba, Wilaya ya Lushoto ameshinda tuzo ya Mfalme Charles III wa Uingereza ijulikanayo kama Prince’s Trust. Tuzo hii ilianzishwa mwaka 2015 na Mfalme Charles III, wakati huo akiwa bado ni mwana wa Mfalme (Prince of Wales), kupitia taasisi yake tanzu iitwayo, Prince’s Trust International.
Zamana amepata tuzo hiyo katika eneo la uwezeshaji wanawake lijulikanalo kama Amal Clooney Women’s Empowerment Award. Bibi Amal Clooney ni mwanasheria wa kimataifa mwenye mafanikio makubwa katika fani yake, ambaye ndiye alimkabidhi Zamana tuzo hiyo.
Taasisi hiyo ya Mfalme Charles III inalenga kuwajengea uwezo vijana wa kike na wa kiume kujifunza, kufanya kazi na kustawi. Tuzo ya Zamana imetokana na kampeni yake ya “Niache Nisome”. Kampeni hii ni ya kuwahamasisha wazazi, jamii na watoto wa kike watumie fursa zilizopo kusoma kwa bidii, kujitunza na kuzingatia masomo kwa ajili ya kujijengea misingi imara ya maisha.
Tarehe 17 Mei 2023, Zamana alikutana na Mfalme Charles III katika Kasri la Buckingham, wakati Mfalme huyo alipofanya dhifa ya kuwapongeza washindi wa tuzo hiyo. Tarehe 19 Mei 2023, Zamana alipokelewa Ubalozi wa Tanzania, London na kufanya mazungumzo na Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro na maafisa wengine wa Ubalozi huo. Zamana anakuwa kijana wa kwanza wa Kitanzania kupata tuzo hiyo adhimu ya kimataifa inayotolewa na taasisi hiyo ya Mfalme Charles III.
Taasisi iliyompendekeza ni Asante Africa Foundation yenye makao yake jijini Arusha, kwa kushirikiana na Prince’s Trust International. Taasisi ya Asante inajishughulisha na uwezeshaji wa vijana katika maeneo ya elimu, stadi za dijitali, ujasiriamali, uongozi na stadi nyingine za maisha.