Pre GE2025 Mtanzania anatekwa nchi jirani hakuna tamko lolote kutoka serikali ya Tanzania, hii ina maana gani?

Pre GE2025 Mtanzania anatekwa nchi jirani hakuna tamko lolote kutoka serikali ya Tanzania, hii ina maana gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Serikali sio mawe ni watu.Nani aoneshe ubinadamu kwani wao wanavyotukana na kudhalilisha viongozi Huwa hawajui Kuna ubinadamu?

Mimi siwezi kuwa mnafiki wa hivyo labda ufanye wewe
Kama wanajua hawawozi wapishe wakae wengine, kuwepo kwenye nafasi hiyo na pamoja na kukubali kukoselewa na kufuata sheria
 
Kama wanajua hawawozi wapishe wakae wengine, kuwepo kwenye nafasi hiyo na pamoja na kukubali kukoselewa na kufuata sheria
Nani akuposhe? Kwani kina maria ndio waliwaingiza? Hawatoi na hakuna Cha kuwafanya na hawapishi.
 
Serikali sio mawe ni watu.Nani aoneshe ubinadamu kwani wao wanavyotukana na kudhalilisha viongozi Huwa hawajui Kuna ubinadamu?

Mimi siwezi kuwa mnafiki wa hivyo labda ufanye wewe
Weka hapa tusi Moja tu ambalo Maria Sarungi aliwahi kumtukana mtu yeyote yule wa ndani ya Serikali.

Halafu ahdabu ya mtukanaji ni kutekwa? Kama ingekuwa hivyo si watu wengi sana wangetekwa?
 
Alaa wewe ni mgeni na Maria Sarungi au siyo?
NImekujibu sehemu ya pili ya swali lako, kuna taratibu za kufuata kama 'wamekashifu', hii ndio inatoa justification ya serikali kitojali watu wake.

Na kiongozi akiwa kwenye nafasi hasimami kama mtu, anasimama kama taasisi, hizi habari za viongozi wana mioyo sijui nyama utupumzishe nazo
 
Nimesikia BBC asubuhi waliyemuhoji alisema watekaji walikuwa ni watanzania wawili na mkenya mmoja kulingana lafudhi zao za kiswahili
 
NImekujibu sehemu ya pili ya swali lako, kuna taratibu za kufuata kama 'wamekashifu', hii ndio inatoa justification ya serikali kitojali watu wake.

Na kiongozi akiwa kwenye nafasi hasimami kama mtu, anasimama kama taasisi, hizi habari za viongozi wana mioyo sijui nyama utupumzishe nazo
Nani asumbuke na hizo taratibu? Unawapuuza Ili siku wakinasa kama hivi ndio wajue hawajui.
 
Nani akuposhe? Kwani kina maria ndio waliwaingiza? Hawatoi na hakuna Cha kuwafanya na hawapishi.
🤣🤣🤣 Mkuu bana utafikiri uko na poda kwa kichwa, kama wako weak hawafai, hicho ndicho taasisi hiyo inachodemand
 
Na wewe Mzee bado uko na fikra za kidingi .. hata baba nyumbani au katika familia huwa ipo kwa ajili yako lakini ukitovuka na kuvuka mpaka ukawa unawasemanga na kuwatukana wanakupoteza mazima. mifano ipo tele.. .ulitaka Maria serikali anayoilipua na kuisinaga kila usiku kasha isimame kutoa neno ! you must be nutt Sio bure.
 
Hizo itifaki ni zipi? Na zinafuatwaje? Na itachukua siku ngapi kukamilika ili Serikali itoe tamko?

Yaani kulaani kutekwa kwa raia wako akiwa nchi jirani Kuna Itifaki?
Mume wa Maria alitoa Taarifa Interpol na Chama Cha Wanasheria wa Kenya hao ndio wamefanikisha Maria kupatikana

Interpol watatumia Taarifa Kwa Serikali Yetu na ndipo tamko litatolewa

Aidha Rais wa LSK ameshawasaliana na mwenzake wa TLS Mh BAK Mwabukusi

Happy New Year 😄
 
Wakuu,

Toka tukio la utekaji wa Maria limetokea jana Januari 12, 2024, akapatikana, akatoa statement kwa ufupi na kusema ataongea vizuri leo hakuna neno lolote kutoka serikali ya Tanzania kuhusu utekaji huo uliofanyika kwa majirani zetu!

Lakini Rais Samia katoa neno jana Simba ilipofuzu kuingia hatua ya Robo Fainali! Mpira una maana sana na tukio la Maria kutekwa ni upuuzi ambao hauhitaji attention ya Rais na Serikali kwa ujumla?

Hii ina maana gani? Serikali imebariki utekaji huo? Wanajua wahusika hivyo hakuna haja ya kuliongelea? Serikali haijali kabisa wananchi wake? Kuna ushirikiano wa vitendo hivi na serikali ya Kenya? Maana kule nako vitendo hivi vimeshamiri karibuni mpaka wakafanya maandano.

Kwanini serikali haijatoa neno lolote kuhusu hili?
Ukiona hakuna kilichoongelewa ujue huyo aliyetekwa hakutekwa kama anavyotaka ifahamike bali kacheza igizo la kujiteka.

Serikali inayo mifumo ya kiusalama yenye kufahamu mengi kuliko sisi tunavyopiga porojo.
 
Hao wanaokashfu Viongozi & Serikali wakitekwa nani awahurumie au kujishughulisha nao? Utakuwa unafiki
Huyo Maria anakwenda mbali zaidi katika kuifanya roho mbaya serikali. Anafikia hatua ya kujiunga pamoja na maadui wa bandari wakiipinga DPW pale bandarini.

Analeta uadui ndani ya Tanzania ambayo Baba yake mzazi alizaliwa akakua mpaka akawa waziri katika awamu ya pili.
 
Back
Top Bottom