Ndali alikuwa barabarani akiendesha gari ya Honda Accord. Alikuwa amesimama kwenye barabara ya kuongozea magari akisubiri igeuke rangi ya kijani aendelee na alikokuwa anakwenda. Meanwhile, mtoto wa miaka 15 (si Mtanzania) akiwa amechukua gari ya rafiki wa kiume wa mama yake (lile Benz) akiwa amempeperushia kandege ka kati polisi, alikuwa anaenda mwenzo wa kasi karibu maili 100 kwa saa.
Ni katika kufukuzana huko na Polisi akaacha njia na kwenda kuligonga ubavuni gari la kina Ndali na jingine yaliyokuwa yanasubiri rangi ya kijani.
Kwa njia Ndali hakuumiia sana ila ule mshtuko uliotokana na impact, bila ya shaka ulisababisha concussion ambayo imeuumiza vibaya ubongo na bila ya shaka kufanya dislocation ya uti wa mgongo. Na hivyo ndivyo vimemuweka kwenye umahututi.
Sijui kama nimefanikiwa kufafanua.