Mtanzania apata ajali Michigan, Mahututi..

Status
Not open for further replies.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina

Ayubu 1:20-22 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka na nchi, na kusujudia akasema, Mimi nilitoka tumboni kwa Mama yangu nili uc*i, nami nitarudi tena huko uc*i vile vile; BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIBARIKIWE. katika mambo hayo yote, Ayubu hakufanya dhambi, wala kumkwaza Mungu kwa upumbavu.

Ayubu 14 1, Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku za kuishi kwake si nyingi, naye hujaa taabu.
 
Apumzike kwa Amani peponi. Mama yake huyo kijana Eva Nzaro alikua balozi wetu India
 
Inasikitisha sana hiki kifo kimenifundisha kuwa tuwe tayari kila wakati maana huwezi jua nini kitatokea!Kwa kweli inauma sana ninapofikiria chanzo cha kifo!MUNGU amuweke mahali pema
mpendwa wetu Marehemu kijana wetu tuliyempenda lakini MUNGU kampenda zaidi!
Poleni sana ndugu wa karibu wa marehemu na watanzania wote!
Ameni!
 
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Ndalima Nzaro - Ameen
 
Mungu ailaze Roho ya Ndalima mahali pema peponi. Mwenzetu anapofariki anatupa pia nafasi ya kukaa na kutafakari maisha yetu, tukijiuliza maswali ya namna tunavyoishi, je tuko tayari??? Hatujui siku wala saa, tujiweke tayari kwa kuishi maisha mema ya kumpendeza mwenyezi Mungu.

Poleni sana wanafamilia wa Nzaro, mtoto wake na mchumba, na marafiki. Shukrani za pekee ziwaendee wale wote waliokuwa wanamuuguza marehemu kwa kipindi kifupi hadi umauti ulipomfika. Na wale waliokuwa wanatuma ujumbe wa faraja kwa wana jf wa huko hasa kuwataka wafanye kila liwezekanalo kumpatia tiba bora. Mungu awe nanyi katika maandalizi ya kuuleta mwili wa marehemu nyumbani kwa mazishi.Mungu awabariki sana.
 
Natanguliza rambirambi kwa familia,ndugu na marafiki wa Ndalima, Mungu ailaze roho ya marehemu peponi. Ameen. Watanzania sote tulio nje tunakuwa wamoja hasa linapotokea jambo la kushikamana kama hili la msiba, kwani kifo hakitabiriki. Ombi kwa mkuu Ab-Titchaz na Mkjj ningeshauri kama inawezekana mkatupatia kiungo kwa mtu aliyeko hapa UK ili sisi tulio hapa tuwasilishe michango yetu? it is more convenient and quicker for those of us who are on this side. Ahsante.
 

The best we could do is to set up the bank account maana we need
all renumerations to go into one pot so as to avoid 'maneno mengi'.
Iwapo you have another idea feel free to let us know and we will do
as best we can from our end.

Asante sana kwako hapo UK, as you omboleza with us here in Michigan.
Mungu akuzidishie nafsi yako.

Regards.
 
Ab-Titchaz,

Wakati tunaendelea kuombeleza ni vizuri pia mkashauriana na familia ya Marehemu kungalia uwezekano wa kuwachukulia hatua za kisheria Polisi waliohusika na hiyo high speed chase.

Katika hali ya kawaida na kulingana na kosa la huyo 15 years ( tunaambiwa aliwaonyesha ishara ya kidole cha kati polisi) halikuhitaji mafukazano yale hususan ktk dunia ya leo ya teknolojia wangeweza ku mtrack na kumpata kirahisi bila ya kusababisha madhara kwa public.

Hapa UK trafick offense ndogo kama hizo polisi huwa wana abandon chase na hasa mtuhumiwa akiwa anaelekea maeneo ya watu wengi, unless awe jambazi ambalo halitakiwi kuwa on the loose hata dakika moja.

Naamini polisi hapo wame act irresponsibly na wana big share of blame. Something should be taken against them.

Naomba kutoa hoja
 
Last edited:

Masatu,

Asante kwa hoja and i can tell you that everything is in play as we speak.
Lakini kwanza kabisa nikumshughulikia marehemu afikishwe nyumbani salama
salmini then we will tackle the nitty gritty of the whole thing.

Regards.
 
Poleni wafiwa na Mungu ailaze pema roho ya mwenzetu.
 

Oh, Lo Lo Lo Lo,
Lo Lo Lo Lo, Lo Lo Lo Lo

Tanzania yateseka
Ndalima Kauawa
Vonetha Kauawa
Walter Kauawa

Ni Mashaka yangaliko
Ndalima kaonewa
Ni Mashaka yangaliko
Ndalima kaonewa

Duniani kitu Wema
Wema haujaonekana
Iliyobaki ni dhuluma
Mabaya ndiyo yatendeka
Hakuna matendo mema
Huruma zimetoweka

Ni Mashaka Yangaliko
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangaliko
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangaliko
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangaliko
Wema Hawana Maisha


Fitina Chuki na Wivu
Dunia imepambika
Yamejaa machukivu
Hayapendezi Hakika
Wema wamepakwa jivu
Hivyo Hawatoanekana

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha


Wema wanapozaliwa
Wema jama wauawa
Tutabaki kuonewa
Tanzania hadi tunyong’onyeke
Wema wangalibakia
Neema tungezipata

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha


Wema wakitaka kuja
Kuja na Kujumuika
Wakailete faraja
Nasi tupate kufarijika
Wakaileta furaha
Nasi tupate kufurahika

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha


Wema Hawana Maisha Jamani, eeeeehe!!

Wema wangalijuwepo
Neema tungezipata
Yasingekuwepo mashaka
Sote tungefurahika
Wema watazidi kuja
Hata wakizuiliwa.

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha

Ni Mashaka Yangalipo
Wema Hawana Maisha


Na Patrick Balisidya
 
Kuhani,

Asante kwa kunifariji mkuu mwenzangu.

Kwa kweli ukijumuisha ile ishu ya Walter na fiance
wake pamoja na hii, basi utaelewa why I have a heavy
heart.I cried for both these brothers coz I just got
overwhelmed asking myself why us?....Hali ya ukiwa ni
ngumu na samtaimu inakufanya ukate tamaa tu.

These senseless deaths have left me even doubting the
purpose of existence bearing in mind that these individuals
were the coolest chaps we had around here.

People going about their business doing everything right kisha
the cruel hand of death comes and scoops them from our midst.

Meanwhile sio kwamba naikosoa kazi ya mungu, lakini jamani.....?
 
Posted by Ab-Titchaz : Meanwhile sio kwamba naikosoa kazi ya mungu lakini jamani.....

.....lakini jamani kazi ya Mungu hapo haieleweki!!
 
Wakuu wote,msiba huu ni mkubwa sana kwetu.Tunaungana na nyie ndugu zetu mlio mlio katika eneo la tukio.Poleni sana na binafsi nimeguswa sana na msiba huu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…