Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Katika khali inayothibitisha ya kuwa fani ya uandishi wa khabari imeingiliwa na kuvamiwa na mamluki wenye nia mbaya ya kushusha hadhi ya vyombo hivyo machoni pa jamii, gazeti la Mtanzania la leo limedai Prof. Lipumba amesema Dr. Slaa hafai kuwa Raisi kwa sababu ni mpenda makundi jambo ambalo siyo la kweli hata chembe.
Katika gazeti la Habari Leo la leo limeweka bayana Prof. Lipumba akimnadi Dr. Slaa kwenye kichwa cha khabari kisemacho "Lipumba asema kama siyo yeye basi ni Dr. Slaa"
Haiwezekani kabisa Prof. Lipumba atoe kauli mbili ambazo zinazotofautiana kiasi hicho........Upande mmoja anamsigina Dr. Slaa na wakati huohuo anamnadi kuwa kwa wale ambao hawapo tayari kumchagua yeye Prof. Lipumba basi kura zao wazielekeze kwa Dr. Slaa ambaye mafanikio yake Bungeni ni ushahidi tosheleza wa kuwa ana nia na uwezo wa kulisaidia taifa hili kuhakikisha "Maisha bora kwa kila Mtanzania."
Gazeti la Mtanzania inashangaza hata watafiti wa "SYNOVATE" hawakulimulika kwa kufanya kazi kiushabiki na wala siyo kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.........Wamiliki wa gazeti hili waone haya na wajirekebishe kwa sababu ni ukweli usiopingika ya kuwa nchi hii bila CCM yawezekana kabisa.................