BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Nyota ya Mtanzania, Gibson Kawago imeendelea kung’ara baada ya kutajwa katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya ubunifu katika uhandisi Afrika inayoratibiwa na Chuo cha Uhandisi cha Uingereza - Royal Academy of Engineering.
Wabunifu watatu wengine wanatoka Nigeria, Afrika Kusini na Uganda wamechaguliwa kushindania Tuzo hiyo inayokuja na kitita cha Pauni 25,000 (Sh milioni 74.6) katika Ubunifu wa Uhandisi.
Shindano hilo limehusisha bunifu ya kubadilisha matumizi ya petroli kwa pikipiki kwa kutumia umeme, kifaa cha kukagua uterasi kinachobebeka, vifurushi vya umeme vilivyotengenezwa kutoka kwenye betri za kompyuta mpakato, na mtandao wa usalama wa kidijitali wa ndani kwa ajili ya usalama wa jamii.
Taarifa iliyotolewa lep Juni 8, 2023 na waandaaji wa Tuzo hiyo binifu hizo zinamanufaa makubwa kama kupunguza gharama za mafuta; kutambua kwa urahisi na kutibu masuala ya afya ya uterasi bila anesthesia; kuzalisha umeme kwa kutumia lithiamu-ion iliyo kwenye betri za kompyuta mpakato kwa ajili ya umeme wa bei nafuu; na kuunganisha jumuiya za wenyeji kupitia mtandao wa uokoaji wa kidijitali ili kuunda vikundi vya polisi vya jamii.
Mshindi wa Tuzo hiyo atatangazwa Julai 6, 2023 jijini Accra na Msindi wa 2 hadi wa nne wote watapata Paundi 10,000 kila mmoja.