Mtanzania hajawahi kumpenda Mtanzania mwenzake. Ushahidi huu hapa chini

Mtanzania hajawahi kumpenda Mtanzania mwenzake. Ushahidi huu hapa chini

UTAJIRI ULIOMO KWENYE MAGROUP YA WHATSAPP

Idadi ya wanakundi zidisha kwa Tsh 1000

Huu ni mchango wa siku moja kwa kila mwanakundi

Kisha zidisha kwa wiki

Kisha zidisha kwa mwezi

Kisha zidisha kwa mwaka

Hapo utaweza kupata jibu la watu waliomakini kwenye kutumia fursa utaona ni kiasi gani cha pesa kwa mwaka wanaweza kukikusanya kama mtaji

Mfano:

▶️Kundi la watu 200

(WNC = 257)

▶️Kila mtu kwa siku atoe 1000

▶️Itakusanywa 200,000

▶️Kwa siku 7 hitakusanywa 1,400,000

▶️Kwa wiki 4 itakusanywa 5,600,000

▶️Kwa mwaka itakusanywa 67,200,000

Jambo hili huweza kufanyika kwa malengo ya mwaka mmoja au miwili kukusanya mtaji

Mradi utakaoanzishwa ukawa na mgao kwa wanakundi kila mwaka

MTAFIKAJE HAPO

▶️Kwanza kundi liwe na watu wenye malengo ya pamoja wakweli waliodhamiria kusaidiana kuondoka kwenye lindi la umasikini

▶️Pili lazima muwe watu wa eneo moja mnaloweza kukutana kwa urahisi

▶️Tatu lazima mfanye mkutano wa pamoja wa maaamuzi ya kuliendea lengo hilo kwa kuchagua viongozi wakweli wenye dira na hilo jambo

▶️Nne lazima ujirasimishe kwa mamlaka husika na kujisajili na muwe na Uongozi na mfungue akaunti ya benki wanakundi wote wawe wanachama wa hiyo taasisi ili waweze kuhoji na kushiriki katika uendeshwaji wa jambo kihalali

Hapa nitakuwa nimewafumbua macho wenye akili

Watu wamo kwenye makundi mengi tu ila hayanafaida zaidi ya kupiga soga kuchekeshana na kutumiana maujingaujinga 🤔

Tuzinduke

Unakuta mtu simu yake ina kundi la:

Shule ya msingi,
Secondary,
A level,
Chuo kikuu,
Bado makundi ya kazini,
Bado makundi ya familia,
Bado makundi ya mitaaani, nk.

Katika makundi haya yote ni liability ya kuomuongezea gharama ya data tu na kusogoa hana kundi hata moja lenye uwezo kumnyanyua kipato chake huku ni kupoteza muda sana🤔🤔

Mwisho wa siku ni umasikini tu uliokithiri🤔

Amkeni, tumelala
 
Ukitaka kuijua vizuri roho ya mtanzania uwe na kigari chako unataka kuingia mainroad kama utapatiwa nafasi, hata zebra kusimama hawataki. Roho mbaya, chuki!
 
Ukitaka kuijua vizuri roho ya mtanzania uwe na kigari chako unataka kuingia mainroad kama utapatiwa nafasi, hata zebra kusimama hawataki. Roho mbaya, chuki!
Mtanzania kila akimwona Mt mwenzake anamwona fursa
 
1. Ni nani aliidhinisha kampuni za bahati nasibu nchini zije zikusanye billions of money kwa Watanzania na kuacha pesa ndogo kwa jina la kodi?
Jibu ni Mtanzania.
2. Ni nani ametoa kibali na ni nani anazifanyia matangazo kampuni za mikopo ya kihuni na kitapeli mitandaoni?
Jibu ni Mtanzania.
3. Nani alipitisha kikokotoo bungeni kinachochukiwa na watumishi zaidi ya laki 5?
Jibu ni Mtanzania.
4. Ni nani alipitisha mikataba ya gesi ya Mtwara ambayo hatusomewi mapato yake au kuelezwa mchango wake kwa uchumi wa Tanzania?
Jibu ni Mtanzania.
5. Ni nani muhujumu wa pesa na Mali za umma?
Jibu ni Mtanzania.
Nani atamdhibiti huyu Mtanzania?
Hii mifano michache inakupa alert, kuwa makini na Mtanzania mwenzako, anaweza kukufanya lolote ilimradi tu atimize adhma yake.
Be straight......
 
Back
Top Bottom