Mtanzania Ibrahim Class amchakaza bondia kutoka Afrika Kusini

Mtanzania Ibrahim Class amchakaza bondia kutoka Afrika Kusini

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253


Bondia Mtanzania, Ibrahim Class usiku wa jana kuamkia leo jumapili Novemba 26 ameandika historia nyingine kwa kutetea ubingwa wa Global Boxing Council (CBG) dhidi ya Bondia Koos Sebiya kutoka Afrika Kusini.

bondia.jpg

Ibrahim Class alishinda kwa pointi 119 dhidi ya pointi 109 za Koos, huku akikiri wazi kuwa mpinzani wake alikuwa amejipanga vya kutosha.

“Halikuwa pambano jepesi, mpinzani wangu alikuwa na nguvu za ajabu, nilipata wakati mgumu hasa kwenye raundi za awali, kama nisingefanya maandalizi ya nguvu basi lolote lingetokea, Koos ni bondia mwenye nguvu sana,” amesema Class baada ya ushindi wa pambano hilo .

Pambano hilo lililohudhuriwa na mamia ya mashabiki kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Class alitwaa taji hilo kwa matokeo ya pointi baada ya kumaliza raundi zote 12 kwenye uzani wa Super feather.

Class ameonyesha uwezo mkubwa kwani mpinzani wake hakuwa bondia legelege, pambano lilikuwa zuri mno na Class katuonyesha kwamba hakubahatisha alipotwaa ubingwa huu kwa mara ya kwanza kule Ujerumani na sasa ameutetea.” alisema Waziri Mwakyembe.

Watanzania waliojitokeza kushangilia walianza kupiga makelele ya shangwe kunako raundi ya tisa baada ya Mtanzania huyo kumtembezea kipigo mpinzani wake ambaye hadi anafika raundi ya 12 tayari alikuwa akivuja damu usoni.
 
Pongezi nyingi kwake kwa ushindi alioupata na kutuwakilisha vyema
 
Pongezi zake nyingi sana,ila onbi langu kwake ASIJIONE SANA KUWA YUPO JUU,KWANI NDO YUPO KTK MAFANIKIO YA CHEKECHEA.
 
Back
Top Bottom