mserekale
Member
- Jul 4, 2019
- 79
- 103
Ni mwaka mwingine wa uchaguzi na kwa desturi ya hapa kwetu Tanzania, uchaguzi hutoa fursa kwa Wananchi kuamua hatma ya maisha yao kwa kuchagua viongozi wa kuwaongoza kila baada ya miaka mitano, ikiisha kiongozi anayekuwa madarakani anaomba ridhaa nyingine ya miaka mitano kukamilisha ungwe ya miaka kumi!
Nngwe ya kwanza ya miaka mitano ilikuwa chini ya daktari mtumbuaji wa majipu, Dr JPM!
Sasa anarudi tena kuomba ridhaa ya miaka mingine mitano kukamilisha ungwe ya pili ya uchaguzi!
Tumejionea hali halisi ya maisha jinsi ilivyokuwa kwa miaka mitano inayomalizika na kila mmoja ni mashuhuda!
Kawaida ungwe ya pili huwa haina mabadiliko yoyote makubwa bali mwendelezo wa yaliyofanyika katika ungwe ya kwanza ya miaka mitano.
Maana yake kwenye uchaguzi huu kama ukichagua CCM umechagua muendelezo ule ule wa maisha yako kama ilivyokuwa kipindi cha miaka mitano inayomalizika.
Kama kipindi cha miaka mitano inayomalizika ulikuwa na maisha mazuri! Uchaguzi huu ukichagua ccm umechagua kuendelea kuishi maisha mazuri kwa miaka mingine mitano.
Kama ni kijana umesota kwa kukosa ajira miaka mitano mfululizo! Ukichagua ccm maana yake umebariki kuendelea kubaki mtaani kwa miaka mingine mitano tena.
Kama ni maskini ukichagua CCM! Umechagua kuishi maisha duni kwa miaka mingine mitano.
Kama ni tajiri ukichagua CCM! Umechagua miaka mingine mitano ya kuishi kwenye ukwasi mkubwa.
Kama ni mtumishi wa umma hujapanda daraja wala kuongezewa mshahara! Ukichagua ccm tafsiri yake ni ndogo kwamba umebariki kuishi bila kuongezewa mshahara kwa miaka mingine mitano!
Kila mtanzania jitathimini kulingana na hali ya kiuchumi na maisha uliyonayo na ufanye uamuzi sahihi October 28, 2020!
Usikubali neno ningejua lije mbele ya safari!