Mtanzania kuwa mzalendo kwa kudai risiti halali ya manunuzi

Mtanzania kuwa mzalendo kwa kudai risiti halali ya manunuzi

Mkuu, yani nimejikuta nakasirika bure nikikumbuka kodi zetu zinavyo fanyiwa anasa kila kona ya kantre.....
Naumia zaidi ninaposikia hadi mifumo ya ulipaji fedha kwa njia za mitandao pia zimechepushwa.....
Nilitaka kufa kabisa baada ya kusikiliza mrejesho kutoka kwa CAG, na wahusika wapo kitaa wanazidi kula bata hata hawajaitwa kuhojiwa...
 
Yaani hata jioni hii nimeweka mafuta ya gari buku 20 sijahangaika kudai risiti ng'oo!
Kodi yenyewe wanakula wale wahuni akina Mwigulu walioruhusiwa kula kwa urefu wa kamba zao...hadi wanavimbiwa!.
 
Uzalendo unatakiwa uanze kuoneshwa na hao wasimamizi wa hizo kodi, Nikomae kulipa kodi halafu wapuuzi wakavuruge hiyo hela?
 
Tamaa ya maisha mazuri ndo inawafanya watu waibe mapato ya serikali ila pia jinsi serikali inavyotumia pesa za walipa kodi nayo inawafanya baadhi ya raia kuona ni haki kuiba wakati si sahihi.

Uko sahihi sana ila nadhani hapa bila automation bro, hakuna tiba, wasomi wakae chini wafanye uchunguzi yakinifu then watengeneze system ambayo italimit kwa kiwango kikubwa wizi. La sivyo ni kama kukimbiza upepo usioonekana.
TRA Tanzania
 
Shida ni kwamba tukishalipa hizo kodi mnajinufaisha wenyewe tu, Matumizi binafsi ya kwenu ni 97%, Matumizi kwaajili ya maendeleo ya walipa kodi 3%, WE KUWEZA??
Ye haogopi??? 😂😂😂😂

Akiwa mkubwa atajua kwanini tunakwepa, kwenye payee tunalia, na bado biasharani tulipe? We sio kweli!
 
Unatupigia kelele kisa serikali hii ya ccm iliyojaa wezi na majambazi kila sehemu 🤔 yani Kila mwaka mabilioni ya fedha ambayo yanatokana na Kodi yanaibwa na watu wachache serikalini alafu hawafanywi Chochote alafu mimi nijisumbue kulipa Kodi ili iweje 🤔 anae kwepa kodi aendelee kukwepa kwa kadri anavyo weza tuu kwa sababu zinako kwenda zinaenda kufaidisha watu wachache tuu
 
Wengine hawadai risiti kwasababu wanajua hata wakilipa Kodi itaishia mikononi mwa mawaziri wachache ambao wataitumia kujinunulia mabasi ya ABIRIA na kuwalipa wachezaji wa timu zao za mpira.
Ingekua hii Kodi inakwenda kununua madawati, kuwalipa walimu vizuri, kununua vifaa tiba na madawa, wengi Sana wangehamasika kulipa Kodi.
 
Back
Top Bottom