Tetesi: Mtanzania Mbaroni Kwa kuiibia Serikali ya Marekani Bilioni 8!

Tetesi: Mtanzania Mbaroni Kwa kuiibia Serikali ya Marekani Bilioni 8!

USA hiyo ishu wanaikomalia sana uzuri wake Mara nyingi kama raia ni mgeni anapata kifungo miaka michache na kufungiwa aruhususiwi kuingia USA kwa muda wa miaka mitano na hiyo kesi dhamana ni ngumu atakaa ikiisha wanamhesabia muda aliokaa na kurudishwa Bongo .Kuna Msenegal alipata kesi kama hiyo aliporudishwa kwao akaja kuishi Cape Town na kufanya mambo huku akisubiri kifungo cha miaka mitano kilipoisha alirudi USA..maana yeye alikua na kesi za kukwepa kodi nyingi kwenye Bank zake alizofungua maeneo tofauti USA...
 
Ndio ila tambua hakuna gereza zuri duniani, alaf unajua kutokana na sheria za huko watamdeport yaani watamrejesha Tz, mm mwenyewe nishawahi kufungwa nchi flan ulaya, miezi 9 tu, but niliisoma namba, wanakilakitu ndani ya gereza, yaani una room yako fresh ndani mna kila kitu kama TV, RADIO, ukitaka unafanya kazi humohumo gerezani wanakulipa kila week kama laki 1 ya Tz, au ukitaka unajiunga na education ukitoka gerezani una certificates zako, ukitaka unacheza mpira wa miguu au basketball, Milo miwili asubuhi na jioni, matibabu kama kawa. Sema kwanza inategemea na nchi, pili ndani ya hio nchi kunategemea na gereza, huku nilioko mm kuna madaraja ya gereza, kwa mfano daraja A) hizo ni gereza mbaya sana kama wauwaji, yaani watu hatari sana, au wenyevifungo vya maisha. Daraja B) ni watu kama wa madawa au wahuni sana kama waliopigana au waliodhuru watu, hili daraja sio zuri pia kama ni mnyonge sana, but ni tofauti sana na A yaani B ni afadhali, daraja C) ni aina ya gereza zuri kidogo, na hii kwa mfano wamekufunga kipindi kirefu B kama miaka 7 au 8 so imebakia miaka miwili kuisha kifungo chako watakuhamisha na kukupeleka C ambako kuna Uhuru zaidi na ni afadhali, daraja D) hili unakua unaachiwa baadhi ya siku kwenda nyumbani kuonana na family na baahi ya siku unarudi kulala gerzani, yaani d ni nusu ya uhuru. Mm nilipekwa C coz kesi yangu ilikua laini sana yaani kiufupi sikua na kosa na baada ya kunifunga walibaini baadae sikua na kosa wakanilipa hela kama Million 4 na nusu za Tz kwa kunieka ndani miezi 9, pia humo humo gerezani nilikua asubuhi naenda kazini wakati jioni naingia education na nilipata certificate na usiku kama SAA 1 naingia Gim baadhi ya siku, sema kuna wazungu kila mda wanawaza kupigana, but yote juu ya yote binaadamu kuwa huru ni muhim sana.
Umekula bata hata hivyo, sio kwa Tz
 
JohnNdungurumedicaidbillingarrest1.jpg



MTANZANIA JOHN NDUNGURU, anayemiliki kampuni ya Mercy Services of Heath inayojishughulisha na kazi ya kuhudumia wagonjwa majumbani (Home Health Care) nchini Marekani, ametiwa mbaroni nchini humo na kufunguliwa mashitaka 12 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Kwa mujibu wa mtandao wa NBCWASHINGTON.COM, ulioandika habari hiyo Desemba 3 mwaka huu, Ndunguru anadaiwa kujipatia kiasi cha dola za Marekani milioni 3.6 (T.shs Bilioni 8) baada ya kuandika nyaraka za madai ya uongo akionesha kuidai serikali ya jimbo la Virginia kiasi hicho akionesha kampuni yake kuhudumia wagonjwa wapatao 59.


Tukio hilo limetokea wakati Jimbo la Virginia linajitayarisha kupanua mpango wa msaada wa tiba na hati za mahakama zinaonyesha kwamba idara inayoshughulikia huduma za tiba tayari imelipa Dola mil. 3.6 kwa kampuni ya Ndunguru.


Trina Greene, ambaye ni meneja katika kampuni hiyo, alisema wafanyakazi walishtushwa na habari hizo, lakini bado wako bega kwa bega na mkuu wao ambaye humwita Dr. John.

Green na wafanyakazi wengine walianza kuhisi dadlili za matatizo wiki iliyopita wakati ofisi yao ilipovamiwa na wapelelezi kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu ambapo kompyuta 10 zilichukuliwa pamoja na masanduku 33 ya hati mbalimbali.


Hati za mahakama zinadai kwamba kulikuwa na saini ya daktari mmoja iliyoghushiwa na rekodi za watu kadhaa waliopata huduma hapo hazionekani zilipo.


Kampuni hiyo hutoa huduma kwa watu wapatao 90 na imeajiri wafanyakazi wapatao 100.


Ndunguru yuko rumande nchini Marekani baada ya kukosa dhamana.
Jamaa ana kesi za kutosha, na za ubakaji
 
Back
Top Bottom