Mtanzania mwenye kuelewa ilipo Mahakama ya Qadhi Mkoani Mbeya tafadhali

Mtanzania mwenye kuelewa ilipo Mahakama ya Qadhi Mkoani Mbeya tafadhali

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Niko mbeya eneo la Tukuyu ninaomba mwenye kujua ilipo Mahakama ya Qadhi anipe uelekeo wa kufika hapo tafadhali
 
Tanzania hatuna mahakama za kadhi!! Kwani Tanzania tokea lini tukaanza kuhukumiwa kwa sheria za kiislam?
 
Tanzania hatuna mahakama za kadhi!! Kwani Tanzania tokea lini tukaanza kuhukumiwa kwa sheria za kiislam?
Ndoa ya Dr. Juma Mwaka Juma na Mkewe Queen Oscar Masanja haijavunjika, limesema Baraza la Ulamaa lililokutana kwa dharura leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni siku chache toka Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam atangaze kuvunjika kwa Ndoa hiyo.

Taarifa ya Baraza hilo kwa Vyombo vya Habari leo imesema baada ya kuliangalia kwa kina swala la Ndoa hiyo limefikia maazimio ya mambo manne ambapo moja ni kuwa Ndoa hiyo haijavunjika hivyo kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika ofisi ya Qadhi, malalamiko hayo au kesi hiyo iendelee katika ofisi ya Qadhi na Baraza la Ulamaa litafuatilia kwa karibu kinachoendelea.

Azimio la pili la Baraza hilo ni kuwafahamisha Waislamu popote pale walipo wasisite kufanya mawasiliano na Baraza la Ulamaa popote pale watakapoona kuna upindishwaji wa mambo huku azimio la tatu likiwa kuwakumbusha kuwa Muhimili wa Mahakama ya Qadhi ni Muhimili muhimu na ungojitegemea hivyo sio sahihi maamuzi yake kuingiliwa na Mamlaka za BAKWATA Wilaya au Mkoa, na pale suala litakaposhindikana katika Mahakama ya chini suala hilo litapanda katika ngazi ya juu ndani ya Muhimili huo na si vinginevyo.

Azimio la nne ni msisitizo wa Baraza la Ulamaa kwamba utaratibu uliowekwa wa mgawanyo wa madaraka kuanzia katika ngazi zote ni muhimu utaratibu huu ukafuatwa na kudumishwa kwa aili ya kuchunga dhana nzuri ya utawala bora ndani ya Baraza.

MWANANCHI
 
Wewe nenda bakwata utapewa maelezo huko
 
Back
Top Bottom