informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 184
- 170
NEW YORK, MAREKANI – Mtanzania Nichesius Godwin amechaguliwa miongoni mwa vijana 15 kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani kushiriki programu ya uongozi na diplomasia ya Umoja wa Mataifa (UN Leadership Immersion 2026). Programu hiyo inafanyika jijini New York kuanzia tarehe Oktoba 19 hadi leo Oktoba 22, 2026, ambako amepata fursa ya kukutana na wanadiplomasia pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za kimataifa.
Kupitia programu hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya The Social Impact Firm, Godwin amefanya mazungumzo na wawakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa kutoka nchi za Rwanda, Brazil, Barbados, Vietnam na New Zealand. Aidha, amekutana na viongozi kutoka shirika la UN Women, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) na taasisi ya Rockefeller Foundation.
Katika mojawapo ya mijadala hiyo, Godwin alizungumza na Megan Gilgan, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimkakati wa UN Women, kuhusu fursa za ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kijamii yanayohudumia wananchi moja kwa moja.
Katika maelezo yake, Gilgan alibainisha kuwa UN Women hushirikiana kwa karibu na serikali, hususan wizara zinazoshughulikia masuala ya jinsia, pamoja na mashirika ya kijamii katika kuendeleza usawa wa jinsia duniani.
Godwin, ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Georgia nchini Marekani, pia ni mwanzilishi wa shirika la DOSO SafeSpace nchini Tanzania. Kupitia nafasi na fursa anazopata, anaendelea kujifunza, kujenga mahusiano ya kimataifa na kutafuta njia za kuchangia maendeleo ya jamii.
Uwezo wake wa kiuongozi ulienda mbali zaidi ambapo mnamo Aprili 2026, alichaguliwa kuwa Rais wa Graduate Student Network, mtandao unaowakilisha wanafunzi wote wa shahada za uzamili na uzamivu katika Chuo Kikuu cha Georgia.
Ushiriki wa Godwin katika programu hii muhimu ya kimataifa hauishii tu kumjenga binafsi, bali unaweka vijana wa Kitanzania katika mwanga wa mijadala ya uongozi na diplomasia ya juu. Maarifa na mahusiano ya kimataifa anayoyapata yanatarajiwa kuimarisha mchango wake katika ustawi na maendeleo ya jamii nchini Tanzania.
Soma: https://www.jamiiforums.com/threads...li-na-uzamivu-chuo-kikuu-cha-georgia.2433689/