Mtanzania Raia wa Marekani anaweza kurithi mali zilizopo Tanzania?

Sio tanzania wageni kibao wanamiliki ardhi bila shida...nliuza shamba langu arusha mateves kwa mzungu mkataba aliandika jina lake....mkewe ni mtanzania ila hakumuweka
Hehehehehehe wewe hilo shamba bado ni lakooo,wewe sio TIC...
 
Mtanzania aliyeko Marekani na ni raia wa kule anaweza kuja kuridhi mali au viwanja vya baba yake aliyeko Tanzania?

Hii imekaaje kisheria?
Diaspora karibu 90% wana ID za Tanzania na Passport za Tanzania.
Ukipata muhtasari wa mtaa kwa laki Moja, kata laki Moja, basi unaweza kununua, kuiuza kusajili ardhi kwa jina lako.
 
Mimi niko fit sana sisi tunajua kutafuta bro ni kweli alinituma niulizie maana ukweli tayari ana viwanja vyake huku sasa yuko kule kakaa miaka30 anataka kurudi bongo.home is best.
Kwani hujaona wazungu wana nyumba zao masaki na siyo raia?
 
Hapa bongo hatuna uraia pacha kwa hiyo ukichukua uraia wa Marekani au nchi yoyote ile, automatically unakuwa umeukana uraia wa Tanzania.

Hivyo kama wewe si raia wa Tanzania utakuwa huna uwezo wa kumiliki ardhi (nyumba, mashamba, kiwanja n.k) ISIPOKUWA utaweza miliki kama muwekezaji tu. Yaani hiyo ardhi itakuwa inamilikiwa na TIC na wewe unakuwa kama mpangaji tu.

Kwa kumalizia huyo ndugu yako unayemuita Mtanzania raia wa Marekani hata weza kurithi hati miliki za mirathi yenye uhusiano na ardhi. Ila atapata mkwanja utokanao na kuuzwa kwa mali za mirathi ihusuyo ardhi. Period.
Nawafahamu wengi sana, tena pasipo kificho chochote wamerithi mali za wazazi wao,wanamiliki ardhi majengo nk! Ni sheria ya vitabuni tu! Nawafahamu vigogo wengi waliofariki na watoto wao wakarithi sehemu za urithi wao pasipo tatizo lolote!
 
Namfahamu jamaa mmoja yuko Canada,sehemu ya urithi wake ilikua katika nyumba, aliirithi na kubadilisha Hati kwa jina lake, kaipangasha na mwanasheria wake anasimamia.
 
Sio katika ardhi..hawezi kurithi mali ambayo inahusisha ardhi kama sio mtanzania.
Wamerithi wengi ndugu yangu,siwezi kukupa orodha,Tanzania yetu ina sheria nyingi danganya toto! Watunga sheria wetu, na vigogo walioko Madarakani na wana watoto wao nje, unadhani hawataki watoto wao wapate matunda ya jasho lao kisa wako nje?
 
Sio katika ardhi..hawezi kurithi mali ambayo inahusisha ardhi kama sio mtanzania.
Mentojo,uko Tanzania? Mojawapo ya kazi yangu katika shirika nililokuwa nikifanya kazi ilikuwa kuwatafutia nyumba za kupanga expatriates, nilikutana na watoto wa vigogo na watanzania wengi wenye nyumba Ada Estates, Mikocheni B, Upanga Masaki huku wakiwa ni raia wa nje, Sheria hiyo unayoisema ni butu,ikitekelezwa itawaumiza hao hao wapishaji.
 
Miaka ya nyuma kabisa nilikutana na kisa hiki,Expatriate toka US alikutana na dada was kihindi ambaye ni real estate agent, akamwambia atamtafutia nyumba Oyster Bay ya kupanga, alichofanya dada huyo alienda serikali akahonga TBA akapangishwa hiyo nyumba, naye akaja kumpangisha huyo mzungu, ni kipindi hata Mkapa hajauza nyumba za serikali. Mchezo huo umefanyika sana,watu kama hao wana guts ya kumnyan'ganya Mtanzania wa kuzaliwa kisa kachukua uraia nje?
 
Kwani mimi mwenye mali hata nikiamua kuachia mali zangu mizimu au taasisi yoyote nani wa kunikataza ?
Nadhani wanachanganya mambo, sipotezi urithi wangu kwa kubadili uraia, narisishwa mali za mzazi wangu kisheria za mirathi,mambo ya sheria za umilikaji wa ardhi ni jambo jingine,na kuna njia nyingi za kui bypass sheria hiyo kisheria...
 
Hapa bongo hatuna uraia pacha kwa hiyo ukichukua uraia wa Marekani au nchi yoyote ile, automatically unakuwa umeukana uraia wa Tanzania.

Hivyo kama wewe si raia wa Tanzania utakuwa huna uwezo wa kumiliki ardhi (nyumba, mashamba, kiwanja n.k) ISIPOKUWA utaweza miliki kama muwekezaji tu. Yaani hiyo ardhi itakuwa inamilikiwa na TIC na wewe unakuwa kama mpangaji tu.

Kwa kumalizia huyo ndugu yako unayemuita Mtanzania raia wa Marekani hata weza kurithi hati miliki za mirathi yenye uhusiano na ardhi. Ila atapata mkwanja utokanao na kuuzwa kwa mali za mirathi ihusuyo ardhi. Period.
Umepotosha mkuu ama umejielekeza vibaya.
 
Mtanzania aliyeko Marekani na ni raia wa kule anaweza kuja kuridhi mali au viwanja vya baba yake aliyeko Tanzania?

Hii imekaaje kisheria?
Inawezekana kabisi mkuu na hii ndio njia PEKEE ambayo mtu asiye raia wa Tanzania atakua na uwezo wa kumiliki ardhi nchini. Ni kwa kupitia URITHI PEKEE mbali na hivyo apitie njia ya uwekezaji.
 
Bexb inawekana na inafanyika na serikali inajua linafanyika, ndio Maana according to Rais Samia alisema vitambulisho maalumu vitawapa hadhi ya kumiliki ardhi,kwa kuwa wanajua linafanyika.
 
Swali gani hili Mkuu? Tumia utashi tu wa kawaida.

Hakuna utashi wa kawaida limekaa kisheria hilo na kuna Precedent ipo ambayo Judge alisema Foreigner anaweza kurithi tena immovable property lakini hii decision inakuwa na ukinzani kwenye sheria za ardhi so swali technical linahitaji mjadala mpana
 
Hapa bongo hatuna uraia pacha kwa hiyo ukichukua uraia wa Marekani au nchi yoyote ile, automatically unakuwa umeukana uraia wa Tanzania.

Hivyo kama wewe si raia wa Tanzania utakuwa huna uwezo wa kumiliki ardhi (nyumba, mashamba, kiwanja n.k) ISIPOKUWA utaweza miliki kama muwekezaji tu. Yaani hiyo ardhi itakuwa inamilikiwa na TIC na wewe unakuwa kama mpangaji tu.

Kwa kumalizia huyo ndugu yako unayemuita Mtanzania raia wa Marekani hata weza kurithi hati miliki za mirathi yenye uhusiano na ardhi. Ila atapata mkwanja utokanao na kuuzwa kwa mali za mirathi ihusuyo ardhi. Period.

Mkuu kuna ile Precedent iliruhusu foreigner kurithi ardhi japo naona judge alijichanganya mana ilikuwa ina contravene land laws vp ilishakuwa over ruled kama unafahamu hilo?
 
Hawezi kurithi kitu chochote Tanzania. Ksbb huyo sio raia wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom