Mshana Jr ukiandika habari za wanga, ulozi, makafara na mambo ya nguvu za kiroho huwa unafiti vizuri sana eneo hilo, lakin mambo ya kisiasa yanakutupa mbali sana mkuu.....unachokifanya unaandika kutokana na mapenzi mazito kwa chama chako ukipendacho (hilo sio tatizo).
Unachofanya ni kujaribu tu kuwalisha watu sumu mbaya kuhusu chama chao ili wakichukie na Rais wao ili wamchukie, jambo ambalo ni gumu kushawishika, ushauri wangu......endelea na uandishi wa masuala uliyo na upeo nayo tu, kuiandika kwa mabaya CCM na mgombea wake ni kupoteza muda bure tu.
Natanguliza samahani kwako mkuu ili nisije kushitakiwa kilingeni nikapigwa kipapai