KERO Mtaro unaharibiwa sababu ya kupitisha malori ya mchanga, anayetuhumiwa na uharibufu huu anajulikana, achukuliwe hatua

KERO Mtaro unaharibiwa sababu ya kupitisha malori ya mchanga, anayetuhumiwa na uharibufu huu anajulikana, achukuliwe hatua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nafikisha lalamiko langu juu ya mkazi huyu wa Mbezi Beach kwa Dokta Hiza.

Huyu bwana anafanya ujenzi wa nyumba yake, na kuacha malori yanayopeleka mchanga na vifaa vya ujenzi yapite hapa kwenye mtaro wakati mtaro huo hauwezi kustahimili uzito huo na kupelekea kuanza kumegua mtaro huo.

Njia nyingine ipo haitumii, lakini analazimisha malori hayo yapite hapo. Kulikuwa na blocks za kuwezesha magari magari madogo na bajaji kupita lakini kutokana na malori hayo kupita palibomoka na kuziba njia na hivyo kusababisha maji kujaa, blocks hizo zilitolewa na malalamiko yalifikishwa kwa kiongozi wa mtaa lakini muhusika akapuuza.

Tunaomba suala hili lishughulikiwe sababu mtaro unaweza kuziba kama akiendelea kutumia njia hiyo na kuleta adha kwenye nyumba zinazonguka eneo hilo.

Asanteni.


photo_1_2024-04-11_01-03-21.jpg
photo_2_2024-04-11_01-03-21.jpg
photo_3_2024-04-11_01-03-21.jpg

hiza.jpg
 
Back
Top Bottom