Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Mgombea Ubunge Jimbo la Ismani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Emmanuela Mtatifikolo ameahidi kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Nyang'oro endapo watakichagua Chama Cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Ismani siku ya Tarehe 1 Juni, 2026.
Ametoa ahadi hiyo wakati wa muendelezo wa kampeni za Uchaguzi katika Jimbo la Ismani wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Nyang'oro waliojitokeza kumsikiliza Mgombea huyo wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Ili kupata mrithi wa Jimbo Hilo ambalo Mbunge wake alifariki Machi 25, 2026.
Soma Pia: Emmanuela Mtatifikolo ajitosa kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Isimani
Pia, Ndugu Mtatifikolo amewaahidi vijana kuwa atakuwa nao pamoja katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo Ufugaji na Kilimo cha Umwagiliaji Kwa kujenga Bwawa kubwa ambalo litasaidia katika Kilimo cha Umwagiliaji pamoja na Kuisaidia mifugo kupata maji na kuwaongezea pesa Kwa vijana hao na Wananchi wote kwa ujumla.