Mtatiro kukusanya saini za wajumbe wa bunge la katiba wanaopinga posho

Mtatiro kukusanya saini za wajumbe wa bunge la katiba wanaopinga posho

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kutoka ukurasa wake wa facebook,Mtatiro ameandika kuwa kuanzia Jumatatu atakusanya saini za wajumbe wa bunge la katiba wanaopinga kuongezwa kwa posho na kisha kumwandikia barua Raisi Kikwete akimuomba asiafiki nyongeza hiyo.Mh.Mtatiro amesema zoezi hilo atakuwa analifanya kila muda wa mapumziko.Amesema siku ya Jumatano ndio ataunganisha sahihi hizo pamoja na hiyo barua na kuiwakilisha kwa mh.Raisi ambae ndio mwenye mamlaka ya kuongeza au kutoongeza hiyo posho.

Mh.Mtatiro ameongeza kuwa yuko teyari kutukanwa,kukejeliwa na hata kupewa majina mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuambiwa anatafuta umaarufu.

Mtatiro amesema kuwa ni bora mara mia moja akatukanwa kuliko kujaza matumbo yao huku mwalimu akilipwa sh 300,000 kwa mwezi!

MY TAKE:
Anastahili pongezi kwa uamuzi huu.
 
Kutoka ukurasa wake wa facebook,Mtatiro ameandika kuwa kuanzia Jumatatu atakusanya saini za wajumbe wa bunge la katiba wanaopinga kuongezwa kwa posho na kisha kumwandikia barua Raisi Kikwete akimuomba asiafiki nyongeza hiyo.Mh.Mtatiro amesema zoezi hilo atakuwa analifanya kila muda wa mapumziko.

Mh.Mtatiro ameongeza kuwa yuko teyari kutukanwa na hata kupewa majina mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuambiwa anatafuta umaarufu.

MY TAKE:
Anastahili pongezi kwa uamuzi huu.

Nilitarajia hili kutokea. Maana kwa wengine ni mtaji wa kujulikana. Hongera kwa kugundua fursa kama hii Mr. Mtatiro.
 
Nitoke vp hii!! ikifika 2015 apate cha kuwadanganya wadanganyika,,,kimoyomoyo anatamani posho ingekua 1 million kwa siku!!!!
 
Atatusaidia kujua nani ni nani.

Hiyo sio kazi iliyompeleka Dodoma, atumie vizuri fursa aliyopewa na rais kutuwakilisha sisi tulio kwenye kundi la watu wenye malengo yanayofanana katika kupata katiba bora. Hayo ya posho amuachie Kashilillah
 
Hiyo sio kazi iliyompeleka Dodoma, atumie vizuri fursa aliyopewa na rais kutuwakilisha sisi tulio kwenye kundi la watu wenye malengo yanayofanana katika kupata katiba bora. Hayo ya posho amuachie Kashilillah

We ndio wale wale!
 
Watanzania tuna matatizo sana.

"The reward of a thing well done, is to have it done." -Ralph Waldo Emerson

Go Mtatiro go! achana na hawa wanaotudanganya kila siku kuwa ni watetezi wetu kumbe ni watetezi wa matumbo yao tu. wabinafis!
 
Hongera Mtatiro kws kuja na suruhisho rahisi kabisa ili tupunguze hizi kelele
 
Kama anatafuta sifa basi sifa hizi ndizo tunazotaka.Tunahitaji watafuta sifa wengi kama hawa na viherehere wa kutosha kuwaunga mkono

Ben Saanane are you for real my young bro?? what about Zitto??
 
Sasa anatumia kanuni gani wakati hata kanuni zenyewe Ndo kwanza zinatengenezwa. Si bora aandike tu kuliko kukusanya saini. Hiyo itakua cut and paste
 
Back
Top Bottom