informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 184
- 170
Waokota taka jijini Dar es Salaam wamehimizwa kujiunga na matawi ya Mtandao wa Waokota Taka Dar es Salaam Rejeshi (MTAWADA) yaliyopo katika mitaa yao, ili kuwezesha kupaza sauti zao dhidi ya changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya changamoto zilizotajwa ni pamoja na kutokueleweka kwa utaratibu wa bei, kunyanyapaliwa na baadhi ya watu katika jamii, hatari ya kupata magonjwa, pamoja na usalama wao kuwa hatarini.
Hayo yalibainishwa na viongozi wa MTAWADA katika semina iliyofanyika Septemba 21, 2025, iliyowakutanisha viongozi wa matawi ya waokota taka kutoka mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mratibu wa MTAWADA, Bw. Athumani Alfred, alisema kundi hilo linakabiliwa na changamoto ambazo bila mshikamano na kupaza sauti kwa pamoja, zinaweza kuchukua muda mrefu kupata ufumbuzi.
Aidha, katika taarifa ya mtandao huo imeelezwa kuwa bei ya taka za plastiki imekuwa ikibadilika kulingana na misimu.
Katika kipindi cha Desemba hadi Februari, bei husimama kwenye Tsh. 100 kwa kilo. Hivyo, mwokotaji anayeweza kuokota kilo 15 kwa siku hupata Tsh. 1,500.
Katika kipindi cha Machi hadi Julai, bei huongezeka na kufikia Tsh. 350 kwa kilo, ambapo mwokotaji hupata hadi Tsh. 5,250 kwa kilo 15.Miezi ya Agosti hadi Oktoba bei hupanda zaidi hadi Tsh. 500 kwa kilo, na mwokotaji wa kilo 15 hupata Tsh. 7,500.
Kufuatia hali hiyo taarifa, MTAWADA imekuwa ikipaza sauti kuhusu changamoto ya bei kupewa uzito ili kupunguza taka za plastiki na kutambua mchango wa wadau hao katika mazingira.