Mtazamo juu ya vijana wa sasa

Kwa hiyo una maanisha machizi watakuwa wengi mno πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
katika harakati za kuelekea Capitalism tutaona mengi...
 
Ni kweli kabsa mkuu lakini unahisi nini kifanyike ili kuondoa hilo tatzo miongoni mwetu vijana maana changamoto ni nyingi sana
Issue ninayo ona inafaa hapa kwa yale niliyoyaona basi vijana wanatakiwa wapewe kipaimbele sana katika jamii zao, wasikilizwe, kwenye kuwasikiliza utapata cha kuwashauri, ninalosema nimeliona mataifa 18 ya ulaya ikiwemo Uingereza, nimekuja Tanzania nimeliona kwa ukubwa, hapa Marekani ndio habari kuu yani vijana wamekuwa tishio kwa siku za usoni..
 
Ningekuwa raisi na power ningemtafuta a man behind the compaign of KATAA NDOA nimsweke ndani ndo chanzo cha yote haya
Sikubaliani na hilo, nimeona ni mfumo wa maisha ndio umeleta haya, kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo wa maisha ya sasa, kuanzia malezi ya nyumbani, elimu, gharama za maisha, utamaduni mpya, na zaidi Umaskini.
 
Umasikini ukizidi unamfanya mtu kuwa fukara na ufukara ukizidi unampelekea mtu kuwa na matatizo ya akili
Matatizo ya afya ya akili yanachukuliwa kama suala la kawaida ila ni janga kubwa na haribifu siku za usoni, tuna kila sababu ya kusimama kupunguza hili katika jamii zetu.. mauaji yataongezeka kutokana na hili, watu kujidhuru wenyewe,watu kuishi maisha mabaya zaidi kwa sababu ya kukata tamaa, yote haya tutayaona siku sii nyingi
 
Kweli tunaelekea pabaya sana siku hizi. Itabidi wazazi wafanye kitu kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
Kwani vijana wenyewe wanasemaje? Tuwasikilize kama ulivyoshauri.
 
Kuna ule utafiti ulifanywa kuhusu Vijana embu utafute unamajibu ya Uzi wako wote huu
Kati ya Vijana 10 ni mmoja tu ndo ana adabu au heshima inayostahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…