Bahati Yakigulu
New Member
- May 22, 2024
- 1
- 1
IKISIRI
Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha mawazo yaliyo katika fikra za binadamu. Kwa mujibu wa Mulokozi (2017), anaianisha aina tatu za Sanaa ambazo ni sanaa ghibu (Muziki na mashairi), sanaa za maonesho (uchoraji, ususi na ufinyanzi) na Sanaa za vitendo (maigizo na tamthiliya). Katika andiko hili linajadili sanaa ya filamu, Sanaa ya muziki na sanaa za maonesho (ulimbwende).
1.MABADILIKO PENDEKEZI KATIKA TASNIA YA FILAMU TANZANIA (BONGO MOVIE)
Miongo miwili imepita tangu tasnia ya filamu (Bongo movie) kuanzishwa nchini Tanzania. Tasnia ya filamu inakadiliwa ilianza miaka ya 1990 na kuchukua mabadiliko ya kuboreka kwa tasnia hii kadri miaka ilivyozidi kwenda. Mnamo mwaka 2005 tasnia ya filamu ilizidi kushika hatamu na kupendwa na Watanzania wengi, waliibuka wasanii chipukizi wa filamu wenye vipaji na badae wakawa nguli kusababisha kuifikisha tasnia ya filamu mpaka mataifa ya Afrika magharibi hususani Nigeria na Ghana. Mwaka 2012 tasnia ya filamu nchini Tanzania ilipoteza mvuto baada ya kufariki kwa baba wa filamu za Kitanzania Steven Charles Kanumba, hadi kufikia sasa tasnia ya filamu nchini Tanzania imepoteza mvuto kwa hadhira wa ndani na nje ya Tanzania. Ili kurudisha na kuendeleza heshima ya filamu nchini Tanzania na kuifanya iendelee ifike mbali nje ya mipaka ya Afrika wadau wa tasnia hii hawana budi kufanya mapinduzi yafuatayo;
Tasnia ya filamu iache kutumia watu maarufu/wenye fedha kupewa uhusika wa kuigiza
Hili ni tatizo kubwa lililoikumba tasnia ya filamu nchini Tanzania, kumekuwepo kwa kasumba ya muda mrefu mchini Tanzania mtu akiwa maarufu au una fedha nyingi anapewa nafasi ya kuigiza bila kujali maudhui ya filamu yaliyokusudiwa jambo ambalo limesababisha tasnia ya filamu kupuuzwa, kupoteza mvuto na kutofatiliwa na hadhira. Waongozaji wa filamu wanadai wakitumia watu hao kazi ya filamu itawafikia wengi Jambo ambalo si la kweli, kwa hiyo wadau wa tasnia ya filamu na bodi ya filamu walithibiti hili tatizo ili filamu za Kitanzania ( Bongo movie) zifanye vizuri kwenye soko la ndani na nje ya Tanzania faida kwa taifa na wasanii kujipatia kipato.
Filamu za Kitanzania (Bongo Movie)zitengenezwe na kusambazwa na makampuni ya kimataifa
Hili ni tatizo kubwa jingine lililofifisha tasnia ya filamu nchini Tanzania, tangu tasnia ya filamu kuanza nchini hakuna filamu iliyotengenezwa na kusambazwa na kampuni la kimataifa jambo ambalo limekosesha hadhi filamu za Kitanzania kutambulika kimataifa kama wafanyavyo mataifa ya Afrika magharibi Nigeria na Ghana wapo kimataifa zaidi. Bodi ya filamu na tasnia ya filamu kwa ujumla wawekeze kwenye makampuni ya kimataifa ya kusimamia filamu Kama vile Lionsgate, Universal, Paramount, 21 Century Fox, na Netflix. Kwa hiyo bodi ya filamu isimamie hili ili kujenga Tanzania ye kesho iliyo nzuri.
Filamu za Kitanzania ziache kuigiza Kama zinaigiza badala ya kuigiza uhalisia
Tatizo kubwa linalorudisha nyuma filamu za Kitanzania wangozaji filamu hawapo makini kutengeneza filamu yenye maudhui yaliyokusudiwa, hii kwa sababu wahusika wa filamu (igizo) hawana uhalisia wa kile wanachokiigizia kwa filamu za Sasa. Hali hii imeteza soko la filamu Kitanzania ndani na nje ya nchi. Bodi ya filamu iweke sheria sio kila mtanzania anaweza kuongoza filamu na kuipandisha kwenye mitandao ya kijamii/runinga itazamwe isipokuwa kuwe na kampuni maalumu iliyopewe mamlaka ndio ziweze kuifanya kazi hiyo. Hii italeta heshima ya filamu za Kitanzania na kuweza kufika mataifa mengine.
Filamu za Kitanzania zisiandaliwe ndani ya muda mfupi
Waongozaji wa filamu za Kitanzania huamdaa filamu ndani ya mwezi mmoja au miwili na kuweza kukamilika jambo ambalo linasababisha kuzalisha kazi za filamu zisizo na ubora wala uhalisia. Wandaaji wa filamu watenge bajeti toshelevu ya kuendeshea utengenezaji filamu katika madhari tofauti tofauti kutokana na maudhui ya filamu. Muda wa kutengeneza filamu ya saa mbili uanzie wala isizidi miaka mitano, wakifanya hivyo uzalishaji wa filamu utakuwa bora na kupendwa kote ulimwenguni.
Picha namba:1
Buriani Steven Charles Kanumba ( 1984-2012) inaaminiwa ndiye Baba wa Tasnia ya Filamu (Bongo Movie) Tanzania, msanii pekee aliyekuwa mwenye mvuto wakati wote kwa hadhira barani Afrika.
Chanzo Cha picha: Google - Wikipedia
2. MABADILIKO PENDEKEZI KATIKA SANAA YA MAONESHO( ULIMBWENDE)
Kwa mujibu wa Wikipedia, shindano la ulimbwende nchini Tanzania kwa mara ya kwanza lilianza mwaka 1967 na washiriki wengi walikuwa wasichana wa mkoa wa Dar es Salaam. Mnamo miaka ya 2000-2010 shindano hili lilishika hatamu kufatiliwa kwa idadi lukuki ya watu na kupendwa takribani Tanzania nzima. Baada ya 2015 mpaka sasa 2024 shindano hili limepoteza mvuto wa kufatiliwa na watu kwa sababu mbalimbali. Kwa hiyo ili shindano hili lirudishe heshima yake na kufanikiwa zaidi tasnia ya Sanaa ya maonesho haina budi kufanya mapinduzi yafuatayo ndani ya miaka 5 ili kuleta mabadiliko ya Tanzania tuitakayo;
Shindano la ulimbwende lisiandaliwe na mtu binafsi/kampuni
Kumekuwepo kwa malamiko mengi kutoka kwa washiriki wa shindano hili kabla na baada ya kutangazwa washindi. Hali hii imesababishwa na kuendeshwa kwa shindano hili mtu binafsi au kampuni, jambo hili limesababisha kuwepo kwa upendeleo wakati wa mchujo/usaili wa washiriki na badae kupatikana kwa washindi wasio na vigezo na Washindi kulalamika kutopewa zawadi walizo ahidiwa. Dosari hii imefanya kupoteza mvuto kwa shindano la ulimbwende nchini Tanzania. Ili kuleta mvuto na haki itendeke kwa kila mshiriki hakuna budi serikali kuendesha shindano hili mwanzo hadi mwisho ili kupambana na uvulivuli wa upendeleo. Wakifanya hivo watapatikana washidi bora kusababisha baada ya miaka mitano (5) kupatikana mlimbwende wa dunia(Miss Tanzania) kutoka nchini Tanzania na hiyo ndio Tanzania tuikayo.
Kamati ya usaili wa ulimbwende itoke nje ya nchi uanachama.
Tasnia ya sanaa ya ulimbwende iunde kamati ya kuratibu na kusimamia shindano la ulimbwende baiana ya nchi uanachama, kwa mfano nchi za Afrika mashariki ziungane ili kundaa kamati hiyo. Kamati itakayoundwa wajumbe wake watakapo patikana wasambazwe miongoni mwa nchi uanachama isipokuwa pasiwe na mjumbe atakaye simamia shindano ndani ya nchi yake. Hii itasaidia kukomeshwa kwa rushwa ya ngono miongoni mwa washirki wa shindano. Tasnia ya ulimbwende ijitathimini hili ili kujenga Tanzaia ya kesho iliyo nzuri.
Mitandao ya kijamii isihusishwe Kama njia ya kutoa maoni ya mashabiki ili kupata washindi
Mitandao ya kijamii ikihusishwa Kama njia ya kutoa maoni ya mashabiki kwa lengo kupata mshindi Kama ilivyo sasa, jambo hili litasabisha majaji kubadili msimamo wao ambapo inasabisha kutoa maamuzi yasio faa hususani kuamua kumtangaza/kuwatangaza washindi. Tasnia ya ulimbwende ikilifanya hili ndani ya miaka mitano (5) mabadiloko yazuri yataonekana.
Picha namba: 2
Wema Issack Sepetu ni mshindi wa ulimbwende (Miss Tanzania ) mwaka 2006. Inaaminiwa ndiye mwanamitindo pekee aliyekuwa na mashabiki lukuki na mvuto kati ya mashindono yate yaliyo wahi kufanyika kabla na baada.
Chanzo Cha picha:
Google - udaku special
MABADILIKO PENDEKEZI KATIKA TASNIA YA MUZIKI
Tasnia ya Muziki nchini Tanzania mpaka Sasa ina miongo miwili na miaka kadha tangu ilipoanza, tasnia hii ina kazi na manufaa mengi kwa jamii tangu kuazishwa kwake ikiwemo kuburudisha, kuelimisha, na kukosoa kupitia ubunifu wa uimbaji wa nyimbo. Tasnia hii tangu kuanza kwake inakuwa kwa kasi sana kupita tasia zote za Sanaa nchini Tanzania pia inafanya vizuri sana kwa soko la ndani. Tasnia hii imeshindwa kufanya vizuri kwenye soko la nje Kama mataifa mengine Nigeria na Afrika Kusini yafanyavyo. Tasnia ya Muziki nchini Tanzania haina budi kufanya mabadiliko yafuatayo ili kufikia Tanzania tuitakayo ndani ya miaka mitano mbele (5), mabadiliko hayo ni kama;
Mu Wasanii wa Kitanzania wawe na meneja wa masoko ya nje.
Wasanii wa Kitanzania walio wengi hawana maneja wa masoko ya nje ya nchi wanao ratibu na kusaidia kutangaza muziki wa nyumbani (Bongo fleva). Mataifa Kama Nigeria na Sauzi Afrika Kusini muziki wao amefika na kusambaa ulimwengu mzima kwa sababu ya kuwekeza maneja wa masoko ya kimataifa. Muziki wa Bongo flava inashindwa kuvuka mipaka ya Tanzania kwa kukosa meneja wa kimataifa licha ya kufanya vizuri nchini Tanzania. Serikali itenge bajeti ndani ya miaka mitano kwa wasanii ili iwakopeshe waweze kuufikisha muziki wa bongo fleva Ughaibuni. Jambo hili linawezekana ndani ya miaka mitano muziki was bongo fleva utafahamika zaidi ya Muziki wa Afrobeat unaoimbwa nchini Nigeria.
Wasanii wasione aibu kujishusha kurudi shule kusoma ili waweze kuendana na ulimwengu wa kisasa
Wasanii wa Kitanzania asolimia 80% hawakubahatika kupata elimu kwa sababu mbalimbali kwa kila mmoja ila baadhi wachache elimu wanao. Chamgamoto wanayoipata wasanii wa Kitanzania kutofahamu lugha hususani ya lugha ya Kiingereza ambayo huwaunganisha na wasanii wa kimataifa funya kazi ya Muziki pamoja, wengi hawafahamu lugha hii kusabibisha kushindwa kufanaya kazi na wasanii wakubwa wa kimataifa licha ya kupata hiyo fursa. Jambo hilo linafifisha tasnia ya Muziki wa bongo fleva kusongo mbele kimataifa. Kwa hiyo suluhisho la tatizo hili wasanii wakirudi shule kusoma huku wakiendelea na kazi ya muziki bila kuacha ndani ya miaka mitano (5) mbele tasnia ya Muziki wa bongo fleva itafika kimataifa kama wasanii wengine wa Nigeria na Sauzi Afrika wanavyong'ara Ughaibuni. Hii itakuwa faidia kubwa kwa msanii, kutangaza taifa na kujipatia kipato.
Kuboresha sheria za hakimiliki na ulinzi wa haki miliki ni muhimu kwa uendelevu na ukuaji wa tasnia ya muziki
Kuimarisha sheria za hakimiliki kunaweza kusaidia katika kulinda kazi za muziki za wasanii na kuhakikisha kwamba wanapokea fidia ya haki kupitia muziki wao. Vilevile itawasaidia kukabiliana na uharamia wa muziki na Ile hali ya watu kudownload (Kupakua) kiholela kazi za wasanii pasipo wasanii wenyewe kunufaika. Sheria ya hakimiliki itasaidia katika kulinda mapato ya wasanii na kukuza mfumo endelevu zaidi wa tasnia ya muziki kwa ndani ya miaka mitano (5).
Picha namba: 3
Diamond Platnumz ( Naseeb Abduli). Inaaminiwa ndiye mwanamuziki wa mfano nchini Tanzania mwenye uwezo wa kuliwakilisha taifa Kimataifa.
Chanzo Cha picha:
Google - Music in Africa
Mwisho, Tasnia ya Sanaa nchini Tanzania iwahimize wasanii kuandaa kazi zao zikilenga walaji wa kazi hizo ulimwengu mzima hususani katika muziki na filamu Kama wafanyavyo Wasanii wa Nigeria na Afrika Kusini ambao ni kama kioo kwetu.
Bahati Yakigulu
Simu: 0762267234
Dar es Salaam

Attachments
Upvote
3