Josephaty Jumapili
New Member
- Feb 1, 2022
- 2
- 0
"Atazamavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo"!
Usemi huu hauchukuliwi katika upana wake japo uhalisia wa maisha ya mtu huanzia katika fikra zake.
Watu wengi wameshindwa kufikia viwango flani vya kiuchumi wakiamini wao sio watu wa kaliba hiyo nakuamini waliofika hatua hizo ni watu baadhi tu wenye sifa kadha wa kadha.
Nguvu ya umasikini huanzia katika fikra,pia nguvu ya utajiri huanzia katika fikra. Msukumo wa ndani juu ya jambo flani hureta vichochezi katika ubongo ambao hutoa tafasri ya uhitaji katika maisha ya mtu hatimae kuchukua hatua ya utekelezaji katika jambo hilo.
Mtazamo ndio huweza kureta badiliko katika fikra za mtu hata akafanya jambo lenye manufaa,lakini kupitia huohuo mtazamo mtu anaweza kushindwa kuishi ndoto zake.
Ili mtu aweze kupata kile anachotaka inategemea anamtazao gani na hicho kitu,si katika swala la mafanikio tu bali hata katika mambo binafsi kama mahusiano nk.
Watu wengi wamekuwa na ndoto nzuri katika maisha yao lakini mtazamo wao juu yamafanikio ya ndoto zao ndiyo yamekuwa uzio wakufikia hatma yao nakujikuta wanaishi tofauti kabisa na matarajio.
Waswahili husema "PENYE NIA,PANA NJIA" hivyo mtu akiamua kutoka moyoni kutekeleza jambo lake 90% anafanikiwa. Jifunze kuzishinda fikra zako zinazokufanya kuona jambo flani huwezi kulipata na kukufanya ubadili malengo.
Mtu alie na mtazamo chanya habadili malengo bali hubadili njia tu ili aweze kufikia malengo yake.

Upvote
0