Mikono yenye Sugu
Senior Member
- Jul 1, 2020
- 133
- 215
Pamoja na kumuunga mkono Mkulu wetu kwa kiasi kikubwa katika maamuzi yake mengi, upenzi wangu haunizuii kuyasemea madhaifu yake kadhaa.
Mara kadha Mkulu akimtambulisha msaidizi wake (Makamu) amekuwa akimsifia kwa "weupe na uzuri". Kwangu hilo linanichefua kwani kwa hadhi na nafasi yake akitoa kauli inakuwa na athari kubwa kwa jamii.
Mathalan, kwa kauli kama hiyo huwa anajiuliza wanawake weusi wanajisikiaje? Bila shaka jambo hilo sio zuri kwani wengine huku mitaani hatuishi kuwajengea "confidence" wanawake weusi wajikubali na wasisumbuke kujichubua kwani uzuri hautafsiriwi kwa weupe au weusi wa mtu.
Tunatoa wito kwa walio karibu na Mkulu, kumshauri juu ya hilo kwani, hata kama anatania, matokeo yake kwa dada zetu ni maumivu mioyoni. Hongereni wanawake wote wa Tanzania, weusi kwa weupe, ninyi ni wazuri na tunawapenda.
Kwa kuwa Mkulu huwa anawasilisha kama "kautani", namshauri pia mama yetu naye amrekebishe kama "kautani" kwa kuwasifia weusi.
Ni hayo tu kwa leo.