Mtazamo wa Mkulu na wanawake weupe

Umewafikiria wanawake weusi waliopo mtaani hujamfikiria mkewe anajisikiaje? Maana kwa jinsi ninavyomuona sio mweupe yule
Pia umemsahau cheusi mangala jembe la mkulu pale bungeni ambalo analitumia kuwavuruga chadema mle mjengoni, namzungumia Tulia
 
Mmmhh
 
Mimi ni mweusi, ila mtu akisifia weupe hata sijisikii vibaya....Cha ajabu mambo mengine huwa najisikia vibaya, sijui kwa nini sijawahi kuona weusi ni tatizo kama watu wengine wanavyotazama

Uko sawa kabisa kwa mtazamo wako. Lakini watu wanatofautiana katika mapokezi na kutafsiri mambo. Saikolojia ya wanawake ni tofauti sana na ile ya wanaume. Ni rahisi mno kumuumiza mwanamke kwa jambo ambalo wewe unadhani ni utani. Mathalan ukikuta mwanamke aliyeachwa na mpenzi wake na kisha mpenzi huyo kunyakuliwa na mwanamke mweupe, aliyeachika atajua kigezo alichokosa ni "weupe". Hapo atafanya kila jitihada naye awe mweupe walao kwa yale maeneo yanayoonekana. Je ulipata kujua kwa nini wanawake wanajichubua?! Waulize watakuambia.
 
Hayo ni mambo ya UTANI kwa ajili ya kusherehesha mikutano. Rais Magufuli ni binadamu kama binadamu wengine wote, suala la utani na kutania watu si kosa eti jamani?

Utani kwa nani? Kafikiria kuwa kwao Zanzibar hakuna mambo ya utani kama hayo? Yeye yule ni mtani wake? Hiyo inaitwa sexism. Kwa nini asiseme Bashe au Zungu Mweupeee mumemuona?
 
Hayo ni mambo ya UTANI kwa ajili ya kusherehesha mikutano. Rais Magufuli ni binadamu kama binadamu wengine wote, suala la utani na kutania watu si kosa eti jamani?
Unashabikia ujingaaaaa! Mke wake anajisikiaje hapo pembeni?
 
Ndio maana mnaongoza kujichubua nyie watz..hahhahahhh
Hii inaitwa inferiority complex ,sijawahi ona kiongozi mwenye low iq hivi....hahhahahhah!
 
Sasa vipi na ile mimba ya yule mtoto ilikuwa ni ya rais wa zimbabwe pia?

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
 
Kwani wanawake weusi ni dosari?!

Me huwa naona weupe ni kama dosari katika jamii ya mwafrika.....!

Mwanamke akiwa mweusi na maji ya kunde halafu awe na shape nzuri huwa ananipa hamasa ya kuvutiwa nae sana kushinda mwanamke mweupe
 
Wewe jiulize mume wa yule mama (kama yupo) huwa anajisikiaje mkewe kuwa karibu na hilo jamaa ?
 
Unapoteza muda kuandika yote haya. Ameshasema yeye ni msukuma na huo ndio udhaifu wao halafu huyo ni mzee wa miaka 60 utaanza vipi kumshauri masuala kama hayo ya wanawake weupe?.
 
Mkuu yupo sawa, wanawake weupe ni wazuri bwana na hata huwa wana roho nzuri. Mkuu yupo sawa kabisaaaa.. ukute demu white alafu shape ya kibantu.. hatari mzeee
 
Mme wa mamaSamia anajisikiaje maana kumsifia mkewa mtu.ni humiliation kwa third parties yaani
Mrs Magu na Mr sulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…