Umeuliza swali zuri sana. Tanzania ikiwa ni moja yanchi za Afrika ni vigumu kuziweka katika karne 10-21, kama ukipima karne kama Nchi za ulaya na marekani zilivyopitia.
Ukiniuliza Tanzania iko karne ya Ngapi, mara moja napiga taswira katika maendeleo, na hapo ndio inakuwa vigumu kuitafutia nafasi Tanzania. Niulize kwa nini?
Sababu ni za wazi kabisa na ni kama zifuatazo:
1. Tanzania inawasomi wengi kuliko Ujerumani, uingereza n.k zilipoanza maendeleo ya viwanda katika karne ya 18.
2. Tanzania ina msukuma mkokoteni aliye na mobile tel inayemrahisishia mawasiliano ambaye muendesha farasi wa ulaya katika karne ya 18 hakuwa naye.
3. Tanzania leo ina 68% ya watanzania wanojua kusoma na kuandika, wakati ambapo kulikuwana 45% ya wafaransa waliojua kusoma wakati wa maendeleo ya viwanda karne ya 18.
4. tanzania inasumbuliwa na njaa kama ulaya ilivyokuwa katika karne ya 19.
5. Usafiri wa kwanza wa gari mshi ulizinduliwa uhispania mwaka 1850, wakati sisi tunalo hilo miaka kibao japo linatuwekaweka.
Nisaidie kuorodhesha mambo mengine kibao ambayo yanaweza kujaza ukurasa huu, bila ya kusahau umeme na mtandao.
Kwa muhtasari ningeweza kusema Tanzania ni nchi iliyokatika karne mchanganyiko, nikimaanisha ina teknolojia za stone age na za kisasa.
Sijui kama nimekujibu swali lako.