Mtazamo Wangu Juu ya Kuinua na Kupika Vipaji vya Michezo Tanzania

Mtazamo Wangu Juu ya Kuinua na Kupika Vipaji vya Michezo Tanzania

Joined
Apr 2, 2012
Posts
75
Reaction score
159
Habari za leo.

Baada ya Tanzania kufungwa na Uganda 1 - 0 katika kuwania tiketi ya kufuzu mashindano ya CHAN, kumeibuka mijadala mingi sana kuhusu kiwango cha timu yetu. Malalamiko mengi yameangukia kwa wachezaji, walimu, TFF, serikali, etc. Naomba niwasilishe maoni yangu kutokana na mimi mwenyewe kuwepo katika michezo Tanzania, pamoja na mtazamo wangu kwa nchi kama Marekani ambapo nimekuwa ninaishi kwa miaka zaidi ya 25 sasa.

Siku zote tulifundishwa kujifunza kutoka kwa aliye na uwezo juu yako, ilihali anakuzidi kifedha, kiakili, nk. Nawasilisha historia yangu ya michezo kwa ufupi kwa sababu itajibu baadhi ya suluhisho ninazopendekeza. Nilikuwa ninacheza mpira wa kikapu (Basketball) kwenye timu ya Vijana (Vijana Basketball Club - VBC) kuanzia 1987 mpaka nipoondoka na kwenda Marekani mwaka 1996. Nilifanikiwa kucheza Umisetta mwaka 1990 na 1991 Zanzibar na Songea (inaweza ikawa 1991 na 1992 - kumbukumbu imenitoka kidogo), nikiitumikia kanda ya Mashariki. Kwenye timu yetu, iliundwa na wachezaji wanaochipukia (nikiwemo mimi), ambao wengi wetu tulikuja kuchezea timu zilizokuwa zinatawala kikapu wakati huo, hususani Vijana na Pazi. Wachezaji kama Patrick Nyembera, Sindila Assey, Gaston Assey, Evarist Mapunda, Peter Bulengelo, Eric Temba, Jenga Mapunda, Paul Kapalata, Atiki Matata, na mimi. Na hii ni kanda ya Mashariki tu. Kulikuwa na wachezaji wengine kutoka kanda zingine pamoja na Zanzibar ambapo walikuwepo akina Dulla na wengineo. Kwenye mpira wa miguu, walikuwepo wachezaji wengi waliokuja kucheza timu za daraja la juu kabisa kama akina Edibily Lunyamila (mmoja wa wachezaji bora kutokea Tanzania. Nilimuona Zanzibar kabla hajawa maarufu. Niljua atakuja kuwa mchezaji bora kabisa), Peter Nkwera, marehemu kocha Banyai, nk. Sababu ya kusema yote haya ni kuonyesha kwamba michezo kama Umisseta illibua wanamichezo wengi bora miaka ya zamani. Kwa bahati mbaya, niliambiwa michezo ya Umisseta ilifutwa (sijui kwa sababu gani). Kipaji kinaibuliwa kama unavyomlea mtoto. Unamtunza, unamlisha, unamvalisha, unamfundisha, na ndio kwa mara nyingi zaidi ndio atakavyokua. Mtoto mwenye malezi na tabia nzuri mara nyingi alipikwa toka udogoni. Sasa kwenye michezo, tunataka kuwapika wakiwa wakubwa. Hii haileti matunda. Unapopanda mahindi, inabidi umwagilie, uulishe, uweke dawa, etc ndio uweze kupata mavuno mengi na mema. Hakuna miujiza.

Michezo inabidi iangaliwe kama sekta zingine za uchumi Tanzania kama tunataka tuwe bora na kuinua uchumi wa wachezaji pamoja na nchi. Kwa ujumla, nchi nyingi zinazofanikiwa kimichezo ni zile zilizowekeza nguvu na fedha kwenye michezo. Hii sio kwa bahati mbaya. Kwa mfano, nikizungumzia mchezo wa kikapu Marekani. Ninaona mfumo wa Umisetta ukitumiwa hapa Marekani. Kuna mashindano ya timu za shule kutoka za msingi, sekondari (grade schools - Pre-School to K-12) mpaka vyuoni (NCAA). Karibu wachezaji wote maarufu wa kikapu wanapatikana kuanzia akina Michael Jordan, Kobe Bryant, Tim Duncan, Shaquille O'Neal, Allen Iverson, LeBron James, etc. Kila mwaka, wachezaji wapya wanazaliwa. Kwahio, ligi ya kikapu Marekani (NBA) haina shida ya kupata wachezaji wenye vipaji wapya. Ndio maana Marekani anatawala mchezo wa kikapu duniani. Makampuni makubwa duniani kama Nike, Adidas, Puma, Reebok, etc. pamoja na makampuni makubwa ya TV kama ESPN, ABC, NBC (kwa hapa Marekani) yanadhamini michezo hii kwa sababu wanaona faida kubwa watakayopata. Kwa hio, wanamichezo wengi wanalipwa fedha nyingi sana. Sio bahati. Ni mipango. Huwezi kupata timu nzuri ya taifa kama hauna misingi mizuri ya kupata vipaji. Kuna viwanja vya kikapu kila shule, kwenye sehemu za kujipumzisha (recreational areas, parks, etc). Thubutu ujaribu ujenge kibanda chako au nyumba uone kitakachokupata kama tunavyofanya nyumbani. Uwanja wa Pazi ulibomolewa na kujengwa hoteli hapo Ohio street. Kutokana na kukua sana kwa michezo Marekani, kumetengeneza ajira kubwa sana (sports industry) - (Sports market size North America 2009-2023 | Statista). Angalia thamani ya timu za michezo mbalimbali Marekani , zinazoweza kuzidi hata uchumi wa nchi nyingi (Sportico Top 150 North American Sports Franchise Valuations).
Kuna wachezaji pamoja na mawakala wa michezo, wahasibu, wakufunzi, wataalamu wa uwekezaji, watunza viwanja, etc. Hao wote wanalipa kodi na wanaajiri watu wengi. Kwahio, serikali ya Marekani wanapata mapato mengi sana pamoja na kuwafaidisha wana michezo.

Wito wangu ni kwamba kama serikali pamoja na sekta binafsi hawatawekeza kwenye michezo kwa nia dhati kabisa, tutakuwa tunabebesha mzigo mkubwa sana wanamichezo. Wamefikia ukomo wao kwa mujibu wa malezi waliyopata. Siwezi kabisa kuwalaumu wachezaji. Mwanafunzi anayesoma zaidi ya wenzake, anayepata mafunzo ya ziada (tuition), aliyelelewa katika familia inayojali elimu, ndiye mara nyingi anayepata mafanikio zaidi. Hakuna tofauti hapo na michezo. Sio kila mTanzania atakuwa Professor, Engineer, Doctor, etc. Michezo ikipewa thamani yake, itazalisha uchumi wake utakaosaidia nchi.

Nawasilisha.

My 2 Cents.
 
Safi, ushauri mzuri sana, tatizo ni umasikini mkuu, huwezi fananisha uchumi wa Tanzania na Marekani, kinachotakiwa ni kujenga academies za michezo
 
Safi, ushauri mzuri sana, tatizo ni umasikini mkuu, huwezi fananisha uchumi wa Tanzania na Marekani, kinachotakiwa ni kujenga academies za michezo
Naomba kwa heshima nitofautiane kidogo na wewe. Ninaelewa tofauti kubwa ya kiuchumi kati ya Marekani na Tanzania. Lakini, hata kwa kidogo kilichopo kinaweza kutumiwa sawasawa kukuza michezo. Ni hatua ndogo ndogo zinaweza kuchukuliwa kama Umisseta na academies kama ulivyosema. Tukiangalia kwa upana na faida zitakazopatkina baadae, fedha zitapatikana.
 
Back
Top Bottom