Mtazamo wangu juu ya yanayoendelea nchini Tanzania kwa sasa

Mtazamo wangu juu ya yanayoendelea nchini Tanzania kwa sasa

6By6 Miguno

Member
Joined
Apr 20, 2025
Posts
75
Reaction score
107
Ikiwa kesho ni siku ambayo kila mmoja wetu anategemea inaenda kuwa siku ndefu isiyotabirika… Huku wengine wakiwa na wasiwasi, Wengine wakiwa very excited pia kuishuhudia maana ni siku yenye utata kuwahi kutokea nchini mwetu kutokana na siasa zetu.

Mtazamo wangu wa kwanza ni kwamba Tanzania haiendi tena kuwa ya kawaida kama ilivyo sasa wala wakati uliopita, Ni wakati ambao naitazama Tanzania yenye mwenendo tofauti kifikira na kimaamuzi… Siwezi kujifanya kuwa naiona kesho halisi kiutabiri hapana ila nasema kutokana na kusoma nyakati na dalili zinazoonekana.

Sifungamani na chama chochote lakini nipende kuwajuza kuwa kwa mtazamo wangu Uchaguzi huu hautazaa matunda mazuri kwa wanaotegemea mambo yataenda sawa kama kawaida ya chaguzi nyingine zilizopita.

Na kama ikatokea watu wakalazimisha ya bora liende basi kimtazamo wangu mimi naona awamu inayotegemea kuwa ya pili ya rais huyu itakuwa ngumu mno kuwahi kutokea chini ya jua hili, Sio ngumu kwa wananchi pekee bali kwake pia kwani hakutakuwa na utulivu na amani tuliyoizoea kabla.

My Quote “Ikitoka hapa salama na CCM Akashika nchi hali ikaendelea kuwa cool kama hakijatokea kitu basi CCM Hatowahi kutoka ikulu” Na hii itakuwa na maana kwamba Bongo sio sehemu ya great thinkers tena better leave the country for the best of your Generations.

Mwisho kabisa kwa mtazamo wangu naona asilimia 90% za mapinduzi even though imezoeleka kuwa Wananchi Watanzania ni waoga ku-react ila kama ni betting mimi naweka dau langu kwenye -Too Much Heavy Reactions
 
Stage ya mwanzo ya mapinduzi tayari imetekelezwa - mwananchi kutambua ulazima wa kubadilisha mwelekeo wa nchi. Hili limo akilini. Stage ya pili ni mapambano -vitongoji, vijiji ,miji na nchi kwa jumla inaasi. Hii Stage ya pili ndio mapinduzi tumezoea kuona kwenye vyombo vya habari vya dunia. Kwa jinsi dunia inavyofatilia kwa karibu uchaguzi huu ,kwa hakika "kutiki"au "kutoka" will be televised and beamed dunia nzima. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom