Mtazamo wangu kuhusu CHADEMA, CCM na Watanzania

mtimawachi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
2,108
Reaction score
3,155
1:Chaguzi Dodoma vs Mlimani city.

Hapa naipongeza chadema kama chama,wajumbe kama watoa maamuzi na wagombea Kwa kuwa kuonyesha utayari wa kupokea matokeo yoyote ambayo wangeyapata.

PONGEZI zaidi ziende Kwa wajumbe wa chadema Kwa kufanya uchaguzi uwe uchaguzi na sio kikao.
HUKU DODOMA Bado tupo kwenye ujinga,woga tamaa,mazoea na unafiki uliokithiri.
Hapa niseme tu CCM ndio inaidumaza Tanzania.

2:Lisu vs CCM
Hapa CCM wameletewa fupa,tutarajie zile siasa za kati ya 2005/2014 kurejea. Siasa zile ndizo CCM ilivuliwa nguo na vilaza wengi wa chama changu waliumbuka. Mbowe Kwa sasa tukubali tu akili ilishagota.

MTAZAMO WANGU hapa Bado chadema wamefaulu na sisi Wana CCM tujiandae Kwa hoja,vitendo na sera imara.Katu tusijiandae Kwa virungu na mabomu.

3:Lisu vs Lisu.
Amepewa matarajio makubwa sana na chama chake,mashabiki na watanzania wengi hasa wanamabadiliko. Ana mlima mrefu sana wa kuwathibitishia wafuasi wake kwamba walikuwa sahihi kumng'oa Mbowe kumweka yeye. Kuna kipindi huyu bwana ana UTOTO Fulani hivi,akiacha UTOTO huo hakika hata ikulu itamfaa:

4: Watanzania.
Hawa ni watu wa hovyo,wakati mwingine huwezi Jua wanataka nini.Mfano wa mambo hayo ni vyeti feki,ushoga rasirimali na viongozi. Namaanisha kiongozi anaweza kuwa mzuri,ila watanzania wakakuangusha

Unaweza ukataka kuleta mabadiliko chanya ambayo watu hawako tayari mayo.

Mwisho niseme tu CCM ni watanzania,upinzani ni watanzania.
Pia tukumbuke wanasiasa sio wa kuwaamini,tukomae wenyewe
 
Sawa naunga mkono mengi hapo ila ni vyema kufahamu kuwa tatizo la CDM halikuwa Mbowe. Kwa hakika kama sio Mbowe tangu 2005 CDM ingekuwa kama CUF, UDP, NCCR na kadhalika. Mbowe amejitoa kwa mali yake na juhudi kubwa mno! Sijui ni Mtanzania gani ameshasahu kuwa Mbowe alitoka jela juzi tu baada ya kukaa huko miezi takriban 6. Na hii sio mara ya kwanza kufungwa, ni zaidi mara ya 4. Halafu utamsikia mtu akisema Mbowe ni chawa wa CCM! Ni watu wa kusamehe tu hawa. Hata mkutano uliofanyika juzi Mbowe ameufadhili kwa fedha zake karibu kila kitu. Sisemi kwamba fedha ni kila kitu la hasha, ila umuhimu wa Mbowe utaonekana siku sio nyingi. Nieleweke naunga mkona mabadiliko kwa dhati, Lissu amekuja sawa ataleta hamasa mpya ila utaniambia kama mwezi April hutasikia watu wakisema afadhali Mbowe arudi. Na hatarudi na si mshauri arudi, aende akapumzike, ana fedha nyingi za kutembea dunia nzima ni wakati wake wa kuinjoy maisha.
 
Mbowe si kwamba ni mbaya,ila ni muda umemuhukumu.Vilevile Lisu so kwamba. ni mzuri sana kuliko Mbowe,ila sasa ni upepo wake
 
Back
Top Bottom