PreGE2025 Mtazamo wangu kuhusu press ya Askofu Gwajima jana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,355
Reaction score
20,792
Jana nimeangalia video ya Askofu Josephat Gwajima kwenye YouTube, na haya ndiyo maoni yangu kuhusu kile alichokisema na alivyokisema.

Kwanza, ni wazi kuwa Gwajima yupo karibu na watu walio ndani ya system yaani watu walioko kwenye vyombo vya dola. Hawa ndio wanaompa taarifa “nyeti” kuhusu yanayoendelea nchini, hususan kuhusu sakata la utekaji na usalama wa taifa.

Gwajima kwa asili ni mpinzani mwenye akili. Marehemu Magufuli hakukosea kumkaribisha ndani ya CCM. Tatizo ni kwamba huenda chama kimeshindwa kumtumia ipasavyo. Watu wa aina ya Gwajima si wale wa kusema “ndiyo mzee” kila mara — wao huona mapengo kwenye mfumo hata kama wengine wanapiga makofi.

Pia soma: Pre GE2025 - Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka

Kwenye mitaa ya Uswahilini, watu kama Gwajima tunawaita “friji haligandishi” wakisikia jambo, wanasema. Hawaogopi kusema ukweli hata kama unamuumiza nani. Wana msimamo, na mara nyingi wana mvuto wa kisiasa kwa wananchi wa kawaida.

Baada ya hiyo press, naamini Gwajima anajua kuwa nafasi yake ya kugombea tena ubunge kupitia CCM imeyumba. Ila hiyo haimaanishi kisiasa amepotea. Kinyume chake — ile press ilikuwa ni mkakati wa kujipanga upya kwa siasa nje ya CCM.

Gwajima ana njaa ya nafasi kubwa zaidi kisiasa. Ni mtu mwenye maono ya juu anajiona kama kiongozi wa juu kabisa wa nchi. Ingawa si rahisi kusema kama ataweza kufika huko, kitu kimoja kiko wazi: Gwajima si mwoga.

CCM wakifanya kosa la kumshughulikia sasa, wakimvua uanachama au kumtishia, wakae wakijua kuwa Gwajima akihamia upinzani — hasa Chadema — mambo yatabadilika.

Chadema wakimpokea na kumruhusu kugombea urais, naamini watajiongezea nafasi kubwa ya kuvuta hisia za wananchi. Gwajima ni msemaji mzuri, ana hoja, na ana uwezo wa kuwasiliana vyema na wananchi kuliko baadhi ya wanasiasa wa upinzani.

Ndiyo, Samia ana nguvu ya chama tawala na huenda akashinda urais, lakini kampeni zitakuwa ngumu. Gwajima anaweza kumpoteza Rais jukwaani kwa hoja na kelele za kisiasa. Lakini kubwa zaidi, anaweza kufanya wabunge wengi wa CCM kupoteza majimbo yao.

Kwa sasa, ushauri wangu kwa CCM ni wamuache kwanza, waache uchaguzi upite. Kujaribu kumzima sasa ni sawa na kumimina petroli kwenye moto unaowaka taratibu.

Mwaka huu wa uchaguzi ni mwaka wa miujiza. Tutarajie mengi. Tukae mkao wa kula muda ndio utakaotoa majibu.
 
Gwajima kama ana ndotoza kuwa rahisi, awe makini sana akiona choo ndotoni asikitumie anaweza kujinyea

Ila Nchi tunahitaji mabadiliko makubwa sana. CCM inatupeleka pabaya
 
Gwaji Boy kashasema ukweli - sasa ni kuamua kusuka ama kunyoa kwa mamlaka ya uteuzi.

Gwaji kawaondoa kwenye lawama vyombo vyote vya ukimzi na usalama wa nchi katika haya mambo ya utekaji, mauaji na udhalilishaji.

Kwa maana hiyo kuna kikundi chenye mamlaka nje ya mifumo ya kawaida ya vyombo vya dola ambacho kinafanya hii kazi ya utekaji na kuua.

Asante Gwaji - hii ndiyo sauti ya watu wengi na hii ndiyo sauti ya Mungu.

Asante kwa kukata utepe.
 
Jana nimeangalia video ya Askofu Josephat Gwajima kwenye YouTube, na haya ndiyo maoni yangu kuhusu kile alichokisema na alivyokisema.

Kwanza, ni wazi kuwa Gwajima yupo karibu na watu walio ndani ya system yaani watu walioko kwenye vyombo vya dola. Hawa ndio wanaompa taarifa “nyeti” kuhusu yanayoendelea nchini, hususan kuhusu sakata la utekaji na usalama wa taifa.

Gwajima kwa asili ni mpinzani mwenye akili. Marehemu Magufuli hakukosea kumkaribisha ndani ya CCM. Tatizo ni kwamba huenda chama kimeshindwa kumtumia ipasavyo. Watu wa aina ya Gwajima si wale wa kusema “ndiyo mzee” kila mara — wao huona mapengo kwenye mfumo hata kama wengine wanapiga makofi.

Kwenye mitaa ya Uswahilini, watu kama Gwajima tunawaita “friji haligandishi” wakisikia jambo, wanasema. Hawaogopi kusema ukweli hata kama unamuumiza nani. Wana msimamo, na mara nyingi wana mvuto wa kisiasa kwa wananchi wa kawaida.

Baada ya hiyo press, naamini Gwajima anajua kuwa nafasi yake ya kugombea tena ubunge kupitia CCM imeyumba. Ila hiyo haimaanishi kisiasa amepotea. Kinyume chake — ile press ilikuwa ni mkakati wa kujipanga upya kwa siasa nje ya CCM.

Gwajima ana njaa ya nafasi kubwa zaidi kisiasa. Ni mtu mwenye maono ya juu anajiona kama kiongozi wa juu kabisa wa nchi. Ingawa si rahisi kusema kama ataweza kufika huko, kitu kimoja kiko wazi: Gwajima si mwoga.

CCM wakifanya kosa la kumshughulikia sasa, wakimvua uanachama au kumtishia, wakae wakijua kuwa Gwajima akihamia upinzani — hasa Chadema — mambo yatabadilika.

Chadema wakimpokea na kumruhusu kugombea urais, naamini watajiongezea nafasi kubwa ya kuvuta hisia za wananchi. Gwajima ni msemaji mzuri, ana hoja, na ana uwezo wa kuwasiliana vyema na wananchi kuliko baadhi ya wanasiasa wa upinzani.

Ndiyo, Samia ana nguvu ya chama tawala na huenda akashinda urais, lakini kampeni zitakuwa ngumu. Gwajima anaweza kumpoteza Rais jukwaani kwa hoja na kelele za kisiasa. Lakini kubwa zaidi, anaweza kufanya wabunge wengi wa CCM kupoteza majimbo yao.

Kwa sasa, ushauri wangu kwa CCM ni wamuache kwanza, waache uchaguzi upite. Kujaribu kumzima sasa ni sawa na kumimina petroli kwenye moto unaowaka taratibu.

Mwaka huu wa uchaguzi ni mwaka wa miujiza. Tutarajie mengi. Tukae mkao wa kula muda ndio utakaotoa majibu.
Kwa hiyo unaitetea CCM?
 
Siasa za Tanzania ni very very predictable.

Nakuhakikishia Gwajiboy ni mmoja wao na ataendelea kuwa mmoja wao, hapa anaandaliwa kiki ya kufukuzwa uanachama ili akagombee CHAUMMA.

Team yake ilianza hizi propaganda mapema, watu tuliozaliwa na IQ za mbali tulijua kitambo watu wako jikoni.
 
Kumwamini Gwajima ambaye anatoka kwenye tawi la mti unaoitwa Sisiem unatakiwa uvurugwe kwanza akili.Ni aina gani ya waovu ambao sisiem haina,ni wanafki,ni waongo,ni wahuni,wapigaji,ni wezi,wenye hila,naweza kusema hakuna aina ya uoavu usiokuwepo.Huyu anakuja kwa hila siasa zake ni kama msukuma mwenzake kule mji wa utalii.Sioni cha kumwamini hata ashushe moto
 
Siasa za Tanzania ni very very predictable.

Nakuhakikishia Gwajiboy ni mmoja wao na ataendelea kuwa mmoja wao, hapa anaandaliwa kiki ya kufukuzwa uanachama ili akagombee CHAUMMA.

Team yake ilianza hizi propaganda mapema, watu tuliozaliwa na IQ za mbali tulijua kitambo watu wako jikoni.
CHAUMA tena sidhani.
 
Jana nimeangalia video ya Askofu Josephat Gwajima kwenye YouTube, na haya ndiyo maoni yangu kuhusu kile alichokisema na alivyokisema.

Kwanza, ni wazi kuwa Gwajima yupo karibu na watu walio ndani ya system yaani watu walioko kwenye vyombo vya dola. Hawa ndio wanaompa taarifa “nyeti” kuhusu yanayoendelea nchini, hususan kuhusu sakata la utekaji na usalama wa taifa.

Gwajima kwa asili ni mpinzani mwenye akili. Marehemu Magufuli hakukosea kumkaribisha ndani ya CCM. Tatizo ni kwamba huenda chama kimeshindwa kumtumia ipasavyo. Watu wa aina ya Gwajima si wale wa kusema “ndiyo mzee” kila mara — wao huona mapengo kwenye mfumo hata kama wengine wanapiga makofi.

Kwenye mitaa ya Uswahilini, watu kama Gwajima tunawaita “friji haligandishi” wakisikia jambo, wanasema. Hawaogopi kusema ukweli hata kama unamuumiza nani. Wana msimamo, na mara nyingi wana mvuto wa kisiasa kwa wananchi wa kawaida.

Baada ya hiyo press, naamini Gwajima anajua kuwa nafasi yake ya kugombea tena ubunge kupitia CCM imeyumba. Ila hiyo haimaanishi kisiasa amepotea. Kinyume chake — ile press ilikuwa ni mkakati wa kujipanga upya kwa siasa nje ya CCM.

Gwajima ana njaa ya nafasi kubwa zaidi kisiasa. Ni mtu mwenye maono ya juu anajiona kama kiongozi wa juu kabisa wa nchi. Ingawa si rahisi kusema kama ataweza kufika huko, kitu kimoja kiko wazi: Gwajima si mwoga.

CCM wakifanya kosa la kumshughulikia sasa, wakimvua uanachama au kumtishia, wakae wakijua kuwa Gwajima akihamia upinzani — hasa Chadema — mambo yatabadilika.

Chadema wakimpokea na kumruhusu kugombea urais, naamini watajiongezea nafasi kubwa ya kuvuta hisia za wananchi. Gwajima ni msemaji mzuri, ana hoja, na ana uwezo wa kuwasiliana vyema na wananchi kuliko baadhi ya wanasiasa wa upinzani.

Ndiyo, Samia ana nguvu ya chama tawala na huenda akashinda urais, lakini kampeni zitakuwa ngumu. Gwajima anaweza kumpoteza Rais jukwaani kwa hoja na kelele za kisiasa. Lakini kubwa zaidi, anaweza kufanya wabunge wengi wa CCM kupoteza majimbo yao.

Kwa sasa, ushauri wangu kwa CCM ni wamuache kwanza, waache uchaguzi upite. Kujaribu kumzima sasa ni sawa na kumimina petroli kwenye moto unaowaka taratibu.

Mwaka huu wa uchaguzi ni mwaka wa miujiza. Tutarajie mengi. Tukae mkao wa kula muda ndio utakaotoa majibu.
Chadema warudi mchezoni then wamchague Gwajima agombee
 
Gwajima ana njaa ya nafasi kubwa zaidi kisiasa. Ni mtu mwenye maono ya juu anajiona kama kiongozi wa juu kabisa wa nchi. Ingawa si rahisi kusema kama ataweza kufika huko, kitu kimoja kiko wazi: Gwajima si mwoga.
Alishasema kitambo nafasi za kisiasa zote ni ndogo sana kwa nafasi aliyonayo
 
Hebu kuwa serious chief! Kweli gwajima awe rais wa JMT? Mtu muongo kama nini!!! Alidanganya vijana wa Kawe kama mazuzu kuwa atawapeleka Japan na atawaletea meli za uvuvi, akwaambia pia atawaletea greda la kukwangua barabara zote jimbo la Kawe. Huyu ni muongo promax.
 
Japan mkafanye nini,wakati huku tuu mnachemka!
 
Gwajima siyo jasiri, katumwa kupima joto la nje kabla hawajatoa wajue wavae makoti ya baridi au t-shirt na kaptura za joto.

Kama anachukia uovu wa ccm ajivue gamba, hapo nitamuona jasiri.

Anachofanya sasa ana tuchungulia kuona huku tukoje kisha anarudi ndani ccm.

Aje mzima tupambane na uovu, kama kuwapopoa mawe ccm tuwapopoe tukiwa huku wao ccm kule.

Lakini yuko ccm anarushaje jiwe akiwa upande huo huo?
 
Back
Top Bottom