Mtazamo wangu kuhusu tangazo la ajira za walimu

Mtazamo wangu kuhusu tangazo la ajira za walimu

Private investigator

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
303
Reaction score
287
Nikiwa kama msomi mpaka sasa naamini mambo yafuatayo kuhusu lile tangazo;
1. Katibu mkuu alitumika kujibu presha ya social network bila scientific evaluation ya reality ofisini kwake.
2. Lile halikuwa tamko rasmi ndiyo sababu lilimezwa na taarifa za chakula mashuleni.
3. Alijua wazi kuwa anawadanganya watanzania.
4. Haukuwa na mawasiliano na hazina kuhusu fedha za kuajiri walimu wapya.
5. Hasingewezi kutoa tamko lingine zaidi ya kusema ajira zipo, hii ni kwasabu ya panya road na wahanga wa JKT na athari za kisiasa.

ATHARI ZA KUTOTIMIZWA KWA TAMKO LA AJIRA
1. Matamko ya Sagini yataanza kupuuzwa hivyo asitumike tena kutoa press release.
2. Vijana wahanga wa kiume watazidisha kunywa pombe na kula ugoro kuondoa stress.
3. Walimu wapya wataanza ajira wakiwa tayari hawana imani na amani kwa serikali ya CCM
4. Wapo watakaokufa ama kwa kujinyonga au kupata ajari baada ya stress.
5. Kuvunjika kwa amani katika ndoa na mahusiano kwa walimu tarajali wanaposhinda net bila ku-socialize na wenzi wao.
6. Madeni kuongezeka kwa wale waliokopa fedha za riba wakitegeme posho za Kuripoti ili watume mpesa kulipa.

KIBAYA ZAIDI NI HIKI
TAMISEMI hawaoni aibu hata kutoona umuhimu wa kuita tena press conference tena ili kutoa tamko ku-update tamko la kukurupuka walilolitoa awali. Wamekaa kimya wakiona ni upuuzi mtupu wakiacha vijana na familia zao gizani.
UNAFIKI WA SIASA ZA UPINZANI NA UDHAIFU WA WAZIRI KIVULI WA ELIMU
Hawa nao wamekaa kimya ilhari watanzania wenzao wapo katika jangwa. Wanajifanya wazalendo huku wakipuuza udhaifu ulio dhairi.
Hakuna cha nani wala nani, wapinzani wote wasakatonge.
Sioni msaada wenu kwa vijana.

NITARUDI TENA, NISUBIRINI
 
Wasiwe na wasiwasi....watapata zawadi ya muungano leo.
 
Mtoto akidanganya anambiwa tabia mbaya nani kakufundisha na viboko anapata, sasa mkubwa kadanganya nani wa kumuadhibu? Tushazoea kuchukulia mambo kirahisi rahisi na kusema watatufanya nini kwanza. Umoja hakuna, inapelekea badala viongozi kuogopa wananchi na kuwanyenyekea, wananchi ndiyo wanaogopa viongozi sasa na kukubali matokeo. Inasikitisha kwa ndugu zetu, jamaa zetu, marafiki zetu wanaosubiria hizo ajira.
 
Kiukweli najisikia kukereka mpaka sijisikii hata kusikia chochote tena. Si kwamba siwezi kuishi bila ajira serikalini, ila kwa kusubiri nilikosubiri na mambo yangu nilivyoyasimamisha ili kujua hatma yangu, najisikia kuichukia serikali hata kama watatoa posti sasa hivi. Nimeshawajua walivyo hivyo nitajua namna ya kwenda nao sawa. Sitalipa kodi yangu yoyote kwa serikali hii ya utendaji huu wa kubahatisha.
Kikubwa ni kuwa WANABAHATISHA ALMOST KILA KITU.
 
Kweli hili jambo limepuuzwa yaani hata vyombo vya habari wapo kimyaa, nimepitia vichwa vya habari vya leo sijaona gazeti lililozungumzia!
Kweli kazi ipo.
 
''...............they are very sensitive to egoism than a camera film to light but slow as tropism to national dvt........''
 
kuna mtu kaanzisha uzi anasema jk kupitia tbc taifa kasema ajira hadi may 28 na ni kwa walimu wa sayans n kweli?
 
Tufute wazo la kuripoti May maana unasababu gani kuamini kuwa hivyo wakati tarehe 25/4/2015 uliamini na haikuwa?
KAMA ULIDANGANYWA APRIL WHY NOT MAY AGAIN?
 
Kiukweli najisikia kukereka mpaka sijisikii hata kusikia chochote tena. Si kwamba siwezi kuishi bila ajira serikalini, ila kwa kusubiri nilikosubiri na mambo yangu nilivyoyasimamisha ili kujua hatma yangu, najisikia kuichukia serikali hata kama watatoa posti sasa hivi. Nimeshawajua walivyo hivyo nitajua namna ya kwenda nao sawa. Sitalipa kodi yangu yoyote kwa serikali hii ya utendaji huu wa kubahatisha.
Kikubwa ni kuwa WANABAHATISHA ALMOST KILA KITU.

Pole sana Private investigator wamaanisha kwa miaka kumi ya usanii wa serikali ya awamu ya nne bado ulikuwa hujaijua? Ukiajiriwa kodi utalipa tu,si hiyari ni wajibu........
 
Last edited by a moderator:
lakini hebu pitieni upya ile taarifa ambayo bado ipo kwenye tovuti ya tamisemi ukisoma paragraph ya nne sentensi ya mwisho kabisa inasema majina yatawekwa kwenye tovuti ya wizara hadi mwishoni mwa mwezi huu, hiyo ndo kauli iliyotumika na km hivyo ndivyo basi bado wapo ndani ya muda!
 
Wasingesema IFIKAPO wangesema KUANZIA TAREHE 25. IFIKAPO maana yake ni kwa tarehe tajwa, not more, no less. Poor gvt.
 
Back
Top Bottom