Binafsi ni mpenzi tu wa muziki, sina taaluma yeyote na masuala ya muziki na ninachoandika hapa ni MTAZAMO wangu binafsi wa kile nilichokiona. Watu wengi wamelalamikia video ya Ali Kiba kutokuwa na uhusiano na kinachoimbwa, hivyo wameingia katika kundi la "wakosoaji".
Binafsi ninapenda kutoa pongezi za dhati kwa Ali Kiba kwa kuwa kwa mara ya kwanza ametoa video na nikaielewa, ni mapinduzi makubwa kwa muziki wake na naamini ni mwanzo mzuri kwake katika utoaji wa video nzuri siku zijazo. Tukija katika hoja ambayo kimsingi ndiyo imesababisha makundi ya wakosoaji na wapongezaji, yaani maudhui ya wimbo kutoonekana kwenye video, nina mtazamo ufuatao;
Kwanza inatakiwa ieleweke kwamba wimbo wa Mwana una mkanganyiko tangu kwenye audio, maudhui ya wimbo yamejaa mafunzo, lawama, huzuni n.k. Lakini beat imechangamka kiasi, ndani ya wimbo kuna kipande cha sebene na vionjo vingine vya kuchangamsha.
Nafahamu lengo la Kiba lilikuwa ni kufikisha ujumbe lakini hakutaka wimbo wake upooze. Laiti kama video ile ingetengenezwa na watayarishaji wetu wa nyumbani ni lazima wangekuwa na traditional way of thinking yaani wangeweka video za huzuni mfano kijana yupo mtaani anataabika alafu mwishoni wakaishia na ali kiba kucheza sebene, hiki ndicho kiunzi ambacho godfather (watengenezaji wa video) wamekiruka.
Godfather wameonyesha ubora wao katika hili na wanahitaji kusifiwa, wamebadilisha dhana nzima ya nyimbo kutoka huzuni na kuwa changamfu, wameifanya video iwe ya kuchezeka zaidi na fun to watch, ninaamini watu watafurahia ile mwana-dance (so fantastic) kuliko idea ya kijana aliyetaabika mtaani.
Walichofanya Godfather ni hiki, kulingana na uchangamfu wa beat na uwepo wa sebene katika nyimbo tayari dhana ya huzuni imekuwa compromised, hivyo wakaamisha focus kutoka kwa "mwana" na mlengwa wa video akawa ni Kiba mwenyewe, yaani msanii anayetaka kufanya onyesho la muziki anafanya mazoezi ya kuimba akiwa bafuni na njiani na kukagua wacheza shoo wake, lakini wimbo unaotumiwa kufanyiwa mazoezi ya kuimba ni huo wa mwana (idea kuu ya wimbo) halafu kile kipande cha sebene ndio onyesho lenyewe.
Hakika dhana hii imefanikiwa.