Mtazamo wangu kuhusu video ya wimbo wa mwana wa Ali Kiba

clinician

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
2,098
Reaction score
4,926
Binafsi ni mpenzi tu wa muziki, sina taaluma yeyote na masuala ya muziki na ninachoandika hapa ni MTAZAMO wangu binafsi wa kile nilichokiona. Watu wengi wamelalamikia video ya Ali Kiba kutokuwa na uhusiano na kinachoimbwa, hivyo wameingia katika kundi la "wakosoaji".

Binafsi ninapenda kutoa pongezi za dhati kwa Ali Kiba kwa kuwa kwa mara ya kwanza ametoa video na nikaielewa, ni mapinduzi makubwa kwa muziki wake na naamini ni mwanzo mzuri kwake katika utoaji wa video nzuri siku zijazo. Tukija katika hoja ambayo kimsingi ndiyo imesababisha makundi ya wakosoaji na wapongezaji, yaani maudhui ya wimbo kutoonekana kwenye video, nina mtazamo ufuatao;

Kwanza inatakiwa ieleweke kwamba wimbo wa Mwana una mkanganyiko tangu kwenye audio, maudhui ya wimbo yamejaa mafunzo, lawama, huzuni n.k. Lakini beat imechangamka kiasi, ndani ya wimbo kuna kipande cha sebene na vionjo vingine vya kuchangamsha.

Nafahamu lengo la Kiba lilikuwa ni kufikisha ujumbe lakini hakutaka wimbo wake upooze. Laiti kama video ile ingetengenezwa na watayarishaji wetu wa nyumbani ni lazima wangekuwa na traditional way of thinking yaani wangeweka video za huzuni mfano kijana yupo mtaani anataabika alafu mwishoni wakaishia na ali kiba kucheza sebene, hiki ndicho kiunzi ambacho godfather (watengenezaji wa video) wamekiruka.

Godfather wameonyesha ubora wao katika hili na wanahitaji kusifiwa, wamebadilisha dhana nzima ya nyimbo kutoka huzuni na kuwa changamfu, wameifanya video iwe ya kuchezeka zaidi na fun to watch, ninaamini watu watafurahia ile mwana-dance (so fantastic) kuliko idea ya kijana aliyetaabika mtaani.

Walichofanya Godfather ni hiki, kulingana na uchangamfu wa beat na uwepo wa sebene katika nyimbo tayari dhana ya huzuni imekuwa compromised, hivyo wakaamisha focus kutoka kwa "mwana" na mlengwa wa video akawa ni Kiba mwenyewe, yaani msanii anayetaka kufanya onyesho la muziki anafanya mazoezi ya kuimba akiwa bafuni na njiani na kukagua wacheza shoo wake, lakini wimbo unaotumiwa kufanyiwa mazoezi ya kuimba ni huo wa mwana (idea kuu ya wimbo) halafu kile kipande cha sebene ndio onyesho lenyewe.

Hakika dhana hii imefanikiwa.
 
u r indeed a great thinker nimekusoma mkuu nimependa ulivyojenga hoja dizaini ungekua mwanasiasa ungetisha!!!
 
waelewa kama wewe wamebaki wachache sn tz hii, guuuud clarification.
 
bora we umewaelewesha tena waambie waache kukremu
 
Wewe ni baadhi ya ma great thinker mnaoifanya JF kubakia kama sehemu bora na makini ya kupata habari na kujifunza vilevile.Hongera sana kwa uchambuzi wako makini.
 
Umeelezea vizuri sana mkuu. Kiukweli nasifu mpango mzima wa video na kila Kitu kilikuwa na maana, na ndio maana video haichoshi kutazama.
Ova
 
kiukweli wewe ndo moja wapo ya ma great thinkers halisi........uchambuzi wako ni yakinifu
 
Wewe ni baadhi ya ma great thinker mnaoifanya JF kubakia kama sehemu bora na makini ya kupata habari na kujifunza vilevile.Hongera sana kwa uchambuzi wako makini.

Umeelezea vizuri sana mkuu. Kiukweli nasifu mpango mzima wa video na kila Kitu kilikuwa na maana, na ndio maana video haichoshi kutazama.
Ova

Watachambia hamira mwaka huu, kumpiga ban Matola walidhani ndio dawa ya kuwahujumu Fans wa Kiba kumbe ndio wamewasha moto hata wale wasomaji wa kimyakimya sasa wameamuwa kuvunja ukimya.
 
Binafsi ni mpenzi tu wa muziki, sina taaluma yeyote na masuala ya muziki na ninachoandika hapa ni MTAZAMO wangu binafsi wa kile nilichokiona. Watu wengi wamelalamikia video ya Ali Kiba kutokuwa na uhusiano na kinachoimbwa, hivyo wameingia katika kundi la "wakosoaji".

Binafsi ninapenda kutoa pongezi za dhati kwa Ali Kiba kwa kuwa kwa mara ya kwanza ametoa video na nikaielewa, ni mapinduzi makubwa kwa muziki wake na naamini ni mwanzo mzuri kwake katika utoaji wa video nzuri siku zijazo. Tukija katika hoja ambayo kimsingi ndiyo imesababisha makundi ya wakosoaji na wapongezaji, yaani maudhui ya wimbo kutoonekana kwenye video, nina mtazamo ufuatao;

Kwanza inatakiwa ieleweke kwamba wimbo wa Mwana una mkanganyiko tangu kwenye audio, maudhui ya wimbo yamejaa mafunzo, lawama, huzuni n.k. Lakini beat imechangamka kiasi, ndani ya wimbo kuna kipande cha sebene na vionjo vingine vya kuchangamsha.

Nafahamu lengo la Kiba lilikuwa ni kufikisha ujumbe lakini hakutaka wimbo wake upooze. Laiti kama video ile ingetengenezwa na watayarishaji wetu wa nyumbani ni lazima wangekuwa na traditional way of thinking yaani wangeweka video za huzuni mfano kijana yupo mtaani anataabika alafu mwishoni wakaishia na ali kiba kucheza sebene, hiki ndicho kiunzi ambacho godfather (watengenezaji wa video) wamekiruka.

Godfather wameonyesha ubora wao katika hili na wanahitaji kusifiwa, wamebadilisha dhana nzima ya nyimbo kutoka huzuni na kuwa changamfu, wameifanya video iwe ya kuchezeka zaidi na fun to watch, ninaamini watu watafurahia ile mwana-dance (so fantastic) kuliko idea ya kijana aliyetaabika mtaani.

Walichofanya Godfather ni hiki, kulingana na uchangamfu wa beat na uwepo wa sebene katika nyimbo tayari dhana ya huzuni imekuwa compromised, hivyo wakaamisha focus kutoka kwa "mwana" na mlengwa wa video akawa ni Kiba mwenyewe, yaani msanii anayetaka kufanya onyesho la muziki anafanya mazoezi ya kuimba akiwa bafuni na njiani na kukagua wacheza shoo wake, lakini wimbo unaotumiwa kufanyiwa mazoezi ya kuimba ni huo wa mwana (idea kuu ya wimbo) halafu kile kipande cha sebene ndio onyesho lenyewe.

Hakika dhana hii imefanikiwa.

Huna ulicho ongea hapa zaidi ya dhana na ulaghai wa maneno
 
Back
Top Bottom