TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,584
Habari wadau,
Awamu iliyopita wengi waliililia katiba mpya sababu utawala uliopita wa awamu ya tano kiukweli uliwabana sana mbavu kila kona mpaka wakajiona kama wao sio sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini SAP baada ya kuingia Mama Samia katika kiti cha Urais kwa kipindi hiki kifupi naona ametosha vya kutosha katika kiti chake cha Urais, amekuwa akiwatendea haki watu wa aina zote bila kujali vyama vyao na Utawala wa Sheria umerudi tena.
Kwa sisi makada imefikia point tunaona kama Mama anawapendelea sana Watoto wa kambo kuliko Watoto wake wa kuwazaa mwenyewe na hii ndio kariba ya Mwanadamu, sasa Wapinzani naamini wamekosa ajenda kilichobaki ni kungoja tu Mama kuwaruhusu kina Tundu Lissu warudi na atawaakikishia ulinzi wa kutosha maana ameshaanza kuwaandalia mazingira ya pakufikia bila shaka.
Sasa katika muktadha kama huu binafsi sioni kama Katiba Mpya ina umuhimu tena, tumuache Mama aendelee tu kutekeleza Ilani ya chama na kile ambacho anakiona sahihi. Wengine wanasema tumuache maama ajiandikie kitabu chake mwenyewe wala tusimshike mkono.
Kuhusu masuala ya tume huru, Uhuru wa vyombo vya habari, Utawala wa haki na Sheria na mengine mengi muachieni Mama najua kwa kipindi kichache wote tumenuelewa anapotupeleka sisi kama Taifa ni pazuri zaidi ya tulipotoka.