Mtazamo wangu, mabadiliko yanayohitajika...

Mtazamo wangu, mabadiliko yanayohitajika...

Katika mambo ambayo ni Magumu kutekelezeka ni haya uliyo ya ainisha hapa Mkuu ,nnaikumbuka kauli aliyowahi kuitoa hadharani na kusema nna mnukuu"atakae jaribu kuuvunja Muungano atavunjika yeye".

Ukijumlisha na Mfumo mzima wa Muundo wa Serikali inayo tokana na Chama Tawala ,Mfumo unao weza kuingiliwa/kutumika na wenye Chama kwa maslahi yao hakika ni ngumu hasa.

Mfano mzuri ni ktk Uchaguzi Mkuu huu wa 2020 na yaliyo tokea ,wenye kutakiwa kusimamia Sheria waliacha jukumu lao na kuungana na Chama dola kuhakikisha Matakwa ya Chama dola yana timizwa kwa gharama yoyote ile.

Poleni sana wapenda Demokrasia ,poleni Wapinzani kwa Vifo/ vilema / Kesi za kubambikiwa na madhila ya kial namna.

R.I.P... Demokrasia ya kweli.
Ni kweli ulivyosema. Ila nachojiuliza kila siku ni kwanini muungano unalindwa kwa gharama ya watu kufa ili hali wananchi wa pande zote hawautaki ubaki ulivyo? Ila kwa maoni yangu nadhani ni sula la muda tu muungano utafutwa na kuanzishwa aina mpya ya ushirikiano. Japo inaweza kuwa ni baada ya muda mrefu lakini mimi sioni viongozi wa CCM wakiweza kuulinda tena kwa muda mrefu sana. Hata CCM inakaribia siku zake za mwisho. Kila nikiangalia kilichotokea kwenye uchaguzi huu uliopita ni wazi kuwa CCM haipendwi tena. Mpaka shemu za vijijini watu wameshaichoka. Kikwazo kiko kwenye dola kuilinda.
 
Back
Top Bottom